Rais na Mwenyekiti wangu Dkt. John Magufuli kamwe usikubali hizi 'Sifa za Kilaana' unazopewa na Viongozi wa Dini hasa wakiwa 'Wanakuombea' mbele yako

Rais na Mwenyekiti wangu Dkt. John Magufuli kamwe usikubali hizi 'Sifa za Kilaana' unazopewa na Viongozi wa Dini hasa wakiwa 'Wanakuombea' mbele yako

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Sina shida na Wewe katika 'Utendaji' wako na unajitahidi japo 'Kibinadamu' bado kuna maeneo mengine hujaweza 'Kukamilisha' na pengine Watanzania tunaokuamini na hata wale waliokuwa hawakuamini nao kwa pamoja katika Uchaguzi huu Mkuu ujao wa tarehe 28 Mwezi Oktoba tukikupa tena 'ridhaa' zetu na 'Kutuongoza' utaweza Kuyakamilisha na Kutufanyia 'Makubwa' Watanzania.

Mheshimiwa Rais Dkt. Magufuli naomba kwa leo tu nikuume kidogo Sikio kwa Kukuomba kabisa acha Kukubali hizi 'Sifa za Kilaana' ambazo naona sasa umekuwa ukipewa sana na Viongozi wa Dini mbalimbali hasa pale wakiwa nawe ama 'Ukumbini' au 'Uwanjani' Kukuombea ( Kufanya Dua ) kwani 'Kiuhalisia' maneno ambayo huwa 'wanakutamkia' sidhani kama unastahili Kuyaamini na Kuyapokea.

Na ukiona hadi leo hii Mpiga Kura wako na Mwana Kampeni wako Kivuli GENTAMYCINE nimekuja na hili Kwako jua ya kwamba halijakaa vizuri si tu Kwako au Kwetu ila nina uhakika hata kwa mwenyewe Muumba ( Mwenyezi Mungu ) nae Kwake 'halifurahii' kwakuwa hizi Sifa zote za 'Kinafiki' ambazo 'nimezibatiza' kuwa 'Sifa za Kilaana' hupaswi Kuzipokea Wewe na wala hazikuhusu kabisa.

Kitendo cha Mchungaji Mmoja leo Kuanza Kukuombea kabla hujaanza 'Kuhutubia' huku akisema haya maneno ninayanukuu hapa.." Ewe Mungu mbariki Kiongozi huyu wa Kipekee kabisa na wa aina yake kuwahi kutokea nchini Tanzania sawa na Malaika "...alikuwa si tu amekukosea Wewe au Sisi Watanzania bali nina uhakika hata Mwenyezi Mungu nae huko juu Mbinguni alikwazika.

Mheshimiwa Rais Dkt. Magufuli labda leo nikuambie tu hapa hapa 'Mubashara' kabisa ni kweli kuwa kwa jinsi Tanzania ilivyokuwa 'Shaghalabaghala' Kiutawala ( Kiuongozi ) tulihitaji Rais wa aina yako ambaye ni Msimamizi, Makini na Mthubutu Kitu ambacho umekiweza kwa kiasi fulani ila Kitendo cha Wewe 'Kusifiwa' kuwa umekuwa bora kuliko wengine GENTAMYCINE nakikataa kwa 100%.

Ukweli utabaki pale pale kuwa hutoweza kuyafikia waliyoyafanya Watangulizi wako Hayati Mwalimu Nyerere, Mzee Mwinyi, Hayati Mkapa na Mzee Kikwete kwani aliyekutangulia amekutangulia tu na hata sasa Wewe 'Kusifiwa' hivi 'Kinafiki' na hawa Viongozi wa Dini 'wanakukosea' mno kwani 'Maendeleo' uyafanyayo sasa 'Misingi' yake mema iliwekwa na hao Watangulizi wako.

Ombi langu tu Kuu Kwako Mheshimiwa Rais hebu 'Kataza' hii tabia ya hawa Viongozi wa Dini ambao leo siogopi kusema kuwa wengi Wao 'Wanaokusifia' wawapo nawe ni 'Wanafiki' watupu na hata tukiwa nao humu 'Mitaani' ndiyo huwa ni 'Vinara' wa Kukusema tena kwa ule 'Mtindo' wa 'Kukuzodoa' kabisa ila wakiwa nawe hapo 'Stejini' hujifanya 'Wanakupenda' na wapo nawe.

Ingekuwa ni Mimi GENTAMYCINE nipo nawe na ni Kiongozi wa Dini halafu nimepewa nafasi ya Kuombea Mkutano wako Sala yangu ingeenda hivi tu..." Ewe Mwenyezi Mungu Mungu wa Ibrahim, Isaka na Yakoko tunashukuru kwa hii Neema yako na Kutukutanisha kwa pamoja hapa. Mbariki Rais wetu huyu na wabariki Wagombea wengine wote wa Nafasi ya Urais nchini Tanzania na kila Mmoja umpe Baraka zako na yule ambaye Watanzania wataona anafaa na kwa nguvu zake Ewe Baba basi aweze Kushinda Uchaguzi huu ujao na aiongoze vyema Tanzania yetu. Iweke Tanzania yetu katika mikono yako Salama na Wabariki pia Watanzania wote popote pale walipo. Wewe Baba ndiyo unamjua Rais wetu ajaye hivyo kama umemchagua miongoni mwa hawa wanaogombea basi Sisi Watanzania tutakushukuru na kumpa Ushirikiano wetu wote bila kujali kama atatokea CCM, CHADEMA au ACT-Wazalendo kwani tunaamini kuwa Wagombea wote hawa ni Wazuri japo wana Uchungu wa kweli na hii Tanzania yetu. Naomba yote haya kwa Jina la Baba, la Mwana na la Roho Mtakatifu "...

Nitashukuru sana Mheshimiwa Rais Magufuli ukiufanyia Kazi 'haraka' huu 'Ushauri' wangu na zikatae hizo 'Sifa' za 'Kinafiki' unazopewa kila mara tu.
 
Ndio maana Lissu anaposema watu hawako huru muelewe. Naamini huyo Mchungaji huwa hatamki maneno hayo akiwa chumbani kwake!
 
hata makonda walimsifia kinafiki saizi hawataki kumuona.

Mkuu nakubaliana kabisa na Wewe kwani majuzi nilikuwepo pale 'Beach Kidimbwi' ambako ndiko ilikuwa moja ya 'Maskani' Kuu ya 'Kula Bata' kwa Paul Makonda huku akiwa na hao 'Marafiki' zake ambao alipokuwa RC walikuwa 'wakimnyenyekea' mno ila kwa jinsi 'walivyobadilika' sasa hadi 'Kumsema' na 'Kumcheka' kweli nimeamini hakuna Watu 'Wanafiki Waandamizi' duniani kama Watanzania hasa ukiwa na Hela au Madarakani.
 
Hapo Magufuli ndio anafurahi sasa kupewa sifa za kulinganishwa na Mungu au wateule wa Mungu (malaika)

Amesha wahi kuitwa mpaka Yesu.
 
Hapo Magufuli ndio anafurahi sasa kupewa sifa za kulinganishwa na Mungu au wateule wa Mungu (malaika)

Amesha wahi kuitwa mpaka Yesu.

Basi ama kuna tatizo Kwake au kwa hao wanaomtamkia hivyo au yawezekana pengine wote wamekutana wana matatizo. Hii Haingii kabisa Akilini.
 
Sauli ufalme akaukosa hivi hivi, Mungu alipoona amekengeuka akampaka mafuta Daudi kupitia Samwel kuwa mfalme huku Sauli akiona roho ya Mungu ikimwacha!
 
Wewe jamaa na johnthebaptist huwa mkiamua kuongea ukweli mnaongea japo u-ccm unawaharibia.

Jana niliamua kufuatilia maombi ya viongozi wa dini kwa makini neno kwa neno ili nipime viwango vyao vya unafiki.

Alianza sheikh akabwabwaja kwa unafiki wa kumtosha, dua yake nikaikadiria 75% ya unafiki;

Akaingia padre wa kikatoliki, alipiga maombi neutrally kama hivyo ulivyopendekeza bila kuuma maneno wala kupindapinda 'ki-ccm ccm', nafikiri Magufuli hakumfurahia hata kidogo kwa kuomba kiongozi yeyote! Hakika maombi yake niliyakadiria 00% ya unafiki;

Akaingia askofu mmoja sijui ni wa kanisa gani yule! Kiwango cha unafiki katika maombi yake hata kumpa 100% bado ni kumpunja.

Tuna viongozi wa dini wa ajabu ajabu sana!
 
Alishasema, "Msinichagulie mgombea wa upinzani, hata kama anafaa"

Hii ni kauli inayoashiria kuwa ameshajitawaza mshindi awali kabla ya yote.

Huyu jamaa ICC The Hague inamuita
 
Tukiangalia utaratibu/mienendo ya kiongozi wetu wa hawamu hii yeye mwenyewe ndie alituaminisha hivyo adi juzi mmoja wa watangulizi wake alipokuja kutufungua macho juu ya kile tulicho aminishwa. Hivyo pamoja na kwamba ushahuri wako ni mzuri lakini je muhusika atauchukulia kama unavyotarajia? Ama na yeye amefurahia dua ya aina hiyo kwa sababu ndivyo anavyo taka watu waamini?

" Ewe Mungu mbariki Kiongozi huyu wa Kipekee kabisa na wa aina yake kuwahi kutokea nchini Tanzania ".
Kwa kuwa kauli hii kiongozi hakuizungumzia kama ilivyokuwa kwenye ile tuzo ya corona, basi naungana na wewe katika ushahuri wako.

"sawa na Malaika ".
Sina uhakika lakini naamini kwamba mchungaji alimaanisha mungu ambariki kiongozi kama anavyo wabariki malaika.
Lakini kama mchungaji alifuata kauli ya kiongozi mwenyewe kwamba anataka hata kesho akienda mbiguni akawangoze malaika, basi pia naungana na wewe katika ushahuri wako.

"Mbariki Rais wetu huyu na wabariki Wagombea wengine wote wa Nafasi ya Urais nchini Tanzania".

Hii ingekuwa ni dua njema na muhimu sana kwa umoja (udugu) wetu wa kitaifa. Lakini katika dua hii sikuungi mkono, na si kwa nia mbaya bali kwa yale ambayo yangekutokea baada ya kuomba dua hii. Tumeaminishwa kwamba baadhi ya wagombea wameingia kwenye kinyang'anyiro hicho kwa uchu wa madaraka, na wengine ni wasaliti wanaotumika na mabeberu, hivyo kuwaombea baraka katika mkutano wa waliotuaminisha hivyo kungekuletea matatizo makubwa na sidhani hata kama ungeruhusiwa kumaliza hayo maombi (dua), ndio maana nimeogopa kukuunga mkono katika hili kwa sababu halingekuwa na mwisho mzuri kwako.
 
Back
Top Bottom