Rais na Mwenyekiti wangu, usisubiri mpaka uharibifu wa Spika Ndugai ukuchafue

Rais na Mwenyekiti wangu, usisubiri mpaka uharibifu wa Spika Ndugai ukuchafue

Tozo za kujenga madarasa haiongelewi tena sijui imekuaje...
Mwigulu amepoa sana kutuletea data za tozo zilizopatikana na zilikoelekea.
Au anaumwa?Kama mzima na anachapa kazi anyoshe mkono juu tumuone tulioko huku BURUNDI
 
Imefikia hatua Spika anamkosoa kila lililo jema na kukubali yasiyofaa. Ukosoaji wa namna hii si afya kwa ustawi wa nchi yetu.

Tabia hii ameanza kuonesha katika hiki cha awamu ya sita. Mbona Rais Magufuli alikuwa anafanya yanayofanywa na awamu hii lakini hakuwahi kukosoa?

Ukosoaji wa aina ya Ndugai ni moja wa ufa hatari sana katika ukuaji wa uchumi na maendeleo ya nchi. Ukiachana na nchi chache sana duniani ambazo zina uchumi imara wa kujiendesha zenyewe, nchi nyingi zinategemea mikopo ili kukamilisha ujenzi.

Spika licha ya kujua umuhimu wa mikopo yenye riba nafuu na masharti rahisi lakini bado anaona mikopo hiyo haifai. Bila kutoa njia mbadala wa kuongeza mapato ya ndani anapinga mikopo nafuu. Je, maendeleo yatakujaje?

Yawezekana Spika kaona siku zake za kukalia kiti cha uspika zimeisha au ana nia na lengo tofauti la kumkwamisha Rais na Mwenyekiti wake.

Rais na Mwenyekiti wangu, nguvu na uwezo wa kumtoa Spika unao, fanya sasa kabla uharibifu wa Spika haujaota mizizi itakayokuwa migumu kuing'oa
Kumtoa Ndugai huo u Spika ni kazi rahisi sana ambayo inaweza kutekelezwa kwa kikao kimoja tu!!
 
serikali ywnye ukomavu wa akili,hubuni namna ya kujipatia pesa zake yenyewe,hubuni uzakishaji wa bidhaa na kutafuta soko nje!! serikali inayopanga miradi kwa kutegemea kukopa tu,ni hatari kubwa!!,
 
Magufuli alikopa 50% ya Deni ndani ya miaka 5
T 21 kwa miaka 5 ndizo alizokopa jiwe, hangaya 11T ndani ya miezi 9.na anasema atakopa ili amalize miradi .mm Sina neno akope lkn kwa mahesabu na matumiz sahh ya hiyo mikopo!!
 
Kumtoa Ndugai huo u Spika ni kazi rahisi sana ambayo inaweza kutekelezwa kwa kikao kimoja tu!!
Siku wakimtoa tu naenda kulipia kadi ya uanachama na malimbikizo yote tangu awamu ya pili ya Kikwete
 
Unashida mahali yaani akikosolewa kidogo unakimbilia mambo ya maumbile so what? Kama hakiwezi why asing’atuke awaache wanaume waashike nchi
Kazi ya uraisi ni ya wanawake,miaka 60 imetutosha.
 
Hahahahahahaaa!! Awamu y 5 ilikua inatuongopea kua miladi yoooote inajengwa kwa kodi zetu.
 
Sasa haya maneno mngemwambia msukuma mwenzenu kipindi kile,maana yeye ndio amevunja rekodi ya kukopa, kwa miaka 5 tu kakopa trillion 30
Lakini miradi mikubwa mikubwa ambayo haijawahi kufanywa na yeyote katika waliomtangulia aliifanya au aliianzisha ambayo ikikamilishwa italeta neema kubwa katika hii nchi, Tugange yajayo ! Mwacheni Jpm legacy yake ni ngumu kuifuta, mark my word !!
 
Back
Top Bottom