Rais na Mwenyekiti wangu, usisubiri mpaka uharibifu wa Spika Ndugai ukuchafue

Rais na Mwenyekiti wangu, usisubiri mpaka uharibifu wa Spika Ndugai ukuchafue

Namuunga mkono spika Ndugai kaongea point tukiichukulia umakini kaongea kitu kizuri kukosea kupo kaamua kujirekebisha
 
Imefikia hatua Spika anamkosoa kila lililo jema na kukubali yasiyofaa. Ukosoaji wa namna hii si afya kwa ustawi wa nchi yetu.

Tabia hii ameanza kuonesha katika hiki cha awamu ya sita. Mbona Rais Magufuli alikuwa anafanya yanayofanywa na awamu hii lakini hakuwahi kukosoa?

Ukosoaji wa aina ya Ndugai ni moja wa ufa hatari sana katika ukuaji wa uchumi na maendeleo ya nchi. Ukiachana na nchi chache sana duniani ambazo zina uchumi imara wa kujiendesha zenyewe, nchi nyingi zinategemea mikopo ili kukamilisha ujenzi.

Spika licha ya kujua umuhimu wa mikopo yenye riba nafuu na masharti rahisi lakini bado anaona mikopo hiyo haifai. Bila kutoa njia mbadala wa kuongeza mapato ya ndani anapinga mikopo nafuu. Je, maendeleo yatakujaje?

Yawezekana Spika kaona siku zake za kukalia kiti cha uspika zimeisha au ana nia na lengo tofauti la kumkwamisha Rais na Mwenyekiti wake.

Rais na Mwenyekiti wangu, nguvu na uwezo wa kumtoa Spika unao, fanya sasa kabla uharibifu wa Spika haujaota mizizi itakayokuwa migumu kuing'oa
Kinachonishangaza maneno kama ya Ndugai yakisemwa na mtu wa upinzani, samia anamfungulia huyo mtu kesi ya ugaidi ila yakisemwa na liccm lenzake anaishia tu kujibizana naye kwnye majukwaa.

Hii nchi dabo standard sijui zitaishi lini ?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Serikali yenye akili husisitiza uzalishaji wa ndani ili iweze kuuza nje na kupata fedha za kigeni. Wanaompotosha mama kwa kopa kopaa kopaaaa kopaaaaaa kopaaaa@aaaaaaaq, sijui wana maana gani.
Tukope kwa tahadhari na kwa viwango.
Ni kweli kukopa siyo jambo zuri sana lakini kwa maslahi ya kiuchumi na udhaifu wa miundo mbinu ni lazima kupata fedha za haraka kutatua shida na mahali pa kupata fedha ni kukopa. Lakini linalotia mashaka kwa wanaomlaumu Rais Samia, ni watu waliokuwepo na walikuwa wakijua kuwa awamu ya tano imekopa zaidi na kwa kificho na wote walinyamaza kimya, na isitoshe hata matumizi mengine mengi hayakuidhinishwa na bunge,na hawakuwahi kuhoji. Na hata ripoti za Cag hazikuwahi kufanyiwa kazi zaidi ya kushuhudia cag mwenyewe anahojiwa na bunge. Kama tunaipenda nchi yetu tuachane na roho ya unafiki haitatufikisha popote.
 
Imefikia hatua Spika anamkosoa kila lililo jema na kukubali yasiyofaa. Ukosoaji wa namna hii si afya kwa ustawi wa nchi yetu.

Tabia hii ameanza kuonesha katika hiki cha awamu ya sita. Mbona Rais Magufuli alikuwa anafanya yanayofanywa na awamu hii lakini hakuwahi kukosoa?

Ukosoaji wa aina ya Ndugai ni moja wa ufa hatari sana katika ukuaji wa uchumi na maendeleo ya nchi. Ukiachana na nchi chache sana duniani ambazo zina uchumi imara wa kujiendesha zenyewe, nchi nyingi zinategemea mikopo ili kukamilisha ujenzi.

Spika licha ya kujua umuhimu wa mikopo yenye riba nafuu na masharti rahisi lakini bado anaona mikopo hiyo haifai. Bila kutoa njia mbadala wa kuongeza mapato ya ndani anapinga mikopo nafuu. Je, maendeleo yatakujaje?

Yawezekana Spika kaona siku zake za kukalia kiti cha uspika zimeisha au ana nia na lengo tofauti la kumkwamisha Rais na Mwenyekiti wake.

Rais na Mwenyekiti wangu, nguvu na uwezo wa kumtoa Spika unao, fanya sasa kabla uharibifu wa Spika haujaota mizizi itakayokuwa migumu kuing'oa
Kuna watu wanafikiria ni kama hawana vichwa

Sent from my Infinix X680 using JamiiForums mobile app
 
Hii inaweza kuwa ni trap,,kuhamisha mjadala..ili ajenda fulani hivi zipite bila maneno...

Ndugai nafikiri anajua anachokifanya...

Muda utasema kweli
 
Tupo na Ndugai mama aache kukopa kopa hovyo pasipokuwa na malengo nchi hii inaweza jiendesha pasipo mikopo siku alitoka madarakani atatiuachia deni la trillion mia maana sio kwa kasi hii miezi tisa ya uongozi wake kakopa si chini ya trillion 10 hadi sasa…
Kesha kopa na hakuna wa kumziwia, huyo ndugai ni mnafiki mkubwa bora akae kimya maana tunamkumbuka Sana maneno na matendo yake enzi za yule bwana, sahizi anajifanya kubwatuka
 
Waliokuwa wakitupeleka vizuri ni awamu ya 5. Ni ngumu kumeza ukweli lakini walikuwa wakituambia ukweli. Uchumi wa kujidanganya kwa mikopo ya hovyo na kutumia hovyo ni kujidanganya ya hali ya juu sana.
kukuambia kwamba wewe ni tajiri ilihali walala na njaa?
 
kukuambia kwamba wewe ni tajiri ilihali walala na njaa?
Kwani mkopo wa WB na IMF unaletea nyumbani kwako? Tunaongelea sustainability ba sovereignty ya nchi hapa. Hatuangalii uvivu wako wa kushindwa kufanya shughuli za kujitafutia kipato.
Nchi inaweza ikawa hoi lakini bado kutakuwepo na individuals wachache wenye ukwasi wa kutisha.
 
E
Mnacheza ngoma ya CCM! CCM mtu hawezi kuongea bila kujua Mkiti anataka nini, Ndugai ni mjumbe wa kamati kuu ya chama, na ni spika, anaaccess ya moja kwa moja na Rais, na sidhani kama inapita wiki moja bila kuongea na Rais! Unadhani anajiongelea tu bila kujua nini anafanya/wanafanya?
Eti tunamihili mitatu.
Huku wakuu wa mihimili ni wajumbe wa vikao vya juu vya chama.
KATIBA MPYA NI SASA,Spika asiwe mbunge toka chama Fulani ili kuondoa ujinga wa mbunge anajivua bungeni spika anamwambia kakae kwa wenzako huku.
 
Dharau tu naona enzi za jiwe kila mtu aliufyata kuanzia kina Mbowe walikuwa kimya over sudden wote wameota mapembe, ndugai yeye alikuwa anasifia tu kila kitu Hadi vya kijinga
Tatizo lako ni Mbowe tu, sio hao wengine.
 
2025 tutashuhudia mengi. Naona Samia nae kaonyesha misuli yake. Kasema ataendelea kukopa. Ila sasa kama wanakopa hizi tozo zetu zinafanya kazi gani ?Au ndo zinawalipa allowances za safari zao.
Hizo tozo zenu ni pesa za mboga tu.
 
Imefikia hatua Spika anamkosoa kila lililo jema na kukubali yasiyofaa. Ukosoaji wa namna hii si afya kwa ustawi wa nchi yetu.

Tabia hii ameanza kuonesha katika hiki cha awamu ya sita. Mbona Rais Magufuli alikuwa anafanya yanayofanywa na awamu hii lakini hakuwahi kukosoa?

Ukosoaji wa aina ya Ndugai ni moja wa ufa hatari sana katika ukuaji wa uchumi na maendeleo ya nchi. Ukiachana na nchi chache sana duniani ambazo zina uchumi imara wa kujiendesha zenyewe, nchi nyingi zinategemea mikopo ili kukamilisha ujenzi.

Spika licha ya kujua umuhimu wa mikopo yenye riba nafuu na masharti rahisi lakini bado anaona mikopo hiyo haifai. Bila kutoa njia mbadala wa kuongeza mapato ya ndani anapinga mikopo nafuu. Je, maendeleo yatakujaje?

Yawezekana Spika kaona siku zake za kukalia kiti cha uspika zimeisha au ana nia na lengo tofauti la kumkwamisha Rais na Mwenyekiti wake.

Rais na Mwenyekiti wangu, nguvu na uwezo wa kumtoa Spika unao, fanya sasa kabla uharibifu wa Spika haujaota mizizi itakayokuwa migumu kuing'oa
umesaha bunge ndo linauwezo wa kumwondoa rais madarakani kwa kumpigia kura.
 
Spika wa Bunge kutoa kauli inayokinzana na Raisi na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi siyo afya njema kwa taifa letu.
-Haya ni matokeo ya Chama Cha Mapinduzi,kumlea Spika kwa vitendo vyake vya utovu wa nidhamu( huko nyuma),
-kwa mfano kuwapokea na kuwakingia kifua Halima Mdee na wenzake -18 ambao hawakuteuliwa na chadema ( kinyume na Sheria ya vyama vya siasa na Uchaguzi,)
-Sheria ya Uchaguzi Tanzania inatambua wabunge wanaotokana na vyama vya siasa na hakuna wabunge binafsi.
-Spika anajiona kuwa yeye anaweza kufanya chochote na hakuna wa kuhoji ndani ya Chama cha Mapinduzi.
-Chama Cha Mapinduzi kilipaswa kumkemea spika kwa kuwakingia kifua Mh. Halima Mdee na wenzake 18, ambao hawatambuliwi na Chedema au chama chochote Cha siasa.
-Kamati ya maadili ya CCM imchukulie hatua za kinidhamu Ndugai kwa kuvunja Sheria zilizopitishwa na bunge hilohilo na kumvunjia heshima Mwenyekiti wa Chama..

Maoni

(1) Miradi hii,ilianza awamu ya tano na ni miradi ya kimkakati, na ni chachu(catalyst) ya shughuli za uchumi na maendeleo ya nchi yetu
(2) Awamu ya tano ilitekeleza miradi hii kwa Mikopo toka taasisi za fedha za ndani na hati fungani kwa fedha za ndani,(
deni liliongezeka kwa asilimia 50.)
(3) Rais SSH yuko sahihi kuendelea kukopa,ili kukamilisha miradi iliyoanzishwa awamu ya tano na mipya.
(4) Miradi hii huwezi kutekeleza kwa maduhuli ya ndani,kwa maana mapato ya ndani asilimia 60 hutumika kulipa mishahara na shughuli za uendeshaji,na asilimia 40 ndiyo hutumika kwenye shughuli za maendeleo
(5).Kuna clip inatembea mitandaoni,ikimuonyesha Spika anapongeza Serikali kukopa fedha za uviko-19 lakini tarehe 28 December 2021 anaonekana akiponda Mikopo (tuwe tunaweka akiba ya maneno).
 
Tupo na Ndugai mama aache kukopa kopa hovyo pasipokuwa na malengo nchi hii inaweza jiendesha pasipo mikopo siku alitoka madarakani atatiuachia deni la trillion mia maana sio kwa kasi hii miezi tisa ya uongozi wake kakopa si chini ya trillion 10 hadi sasa…
Acha uzushi na propaganda za kijinga, takwimu za kukopa hiyo trillion 10, umezitoa wapi? Deni la Taifa hadi Sasa no trillion 72. Magufuli aliacha deni la Taifa likiwa trl.71, Kiwete aliacha likiwa trl.43. Kama Samia angekuwa kakopa trl.10 Kama unavyo dai deni Taifa lingekuwa trl 80+.
 
Back
Top Bottom