Imefikia hatua Spika anamkosoa kila lililo jema na kukubali yasiyofaa. Ukosoaji wa namna hii si afya kwa ustawi wa nchi yetu.
Tabia hii ameanza kuonesha katika hiki cha awamu ya sita. Mbona Rais Magufuli alikuwa anafanya yanayofanywa na awamu hii lakini hakuwahi kukosoa?
Ukosoaji wa aina ya Ndugai ni moja wa ufa hatari sana katika ukuaji wa uchumi na maendeleo ya nchi. Ukiachana na nchi chache sana duniani ambazo zina uchumi imara wa kujiendesha zenyewe, nchi nyingi zinategemea mikopo ili kukamilisha ujenzi.
Spika licha ya kujua umuhimu wa mikopo yenye riba nafuu na masharti rahisi lakini bado anaona mikopo hiyo haifai. Bila kutoa njia mbadala wa kuongeza mapato ya ndani anapinga mikopo nafuu. Je, maendeleo yatakujaje?
Yawezekana Spika kaona siku zake za kukalia kiti cha uspika zimeisha au ana nia na lengo tofauti la kumkwamisha Rais na Mwenyekiti wake.
Rais na Mwenyekiti wangu, nguvu na uwezo wa kumtoa Spika unao, fanya sasa kabla uharibifu wa Spika haujaota mizizi itakayokuwa migumu kuing'oa