Rais na Mwenyekiti wangu, usisubiri mpaka uharibifu wa Spika Ndugai ukuchafue

Rais na Mwenyekiti wangu, usisubiri mpaka uharibifu wa Spika Ndugai ukuchafue

Waliokuwa wakitupeleka vizuri ni awamu ya 5. Ni ngumu kumeza ukweli lakini walikuwa wakituambia ukweli. Uchumi wa kujidanganya kwa mikopo ya hovyo na kutumia hovyo ni kujidanganya ya hali ya juu sana.
Ukweli kwamba walikuwa HAWAKOPI?
 
Unashida mahali yaani akikosolewa kidogo unakimbilia mambo ya maumbile so what? Kama hakiwezi why asing’atuke awaache wanaume waashike nchi
Dharau tu naona enzi za jiwe kila mtu aliufyata kuanzia kina Mbowe walikuwa kimya over sudden wote wameota mapembe, ndugai yeye alikuwa anasifia tu kila kitu Hadi vya kijinga
 
Ukosoaji si afya kwa ustawi wa Taifa??? lazima umekula maharage mabovu wewe
 
  • Thanks
Reactions: Ame
2025 tutashuhudia mengi. Naona Samia nae kaonyesha misuli yake. Kasema ataendelea kukopa. Ila sasa kama wanakopa hizi tozo zetu zinafanya kazi gani ?Au ndo zinawalipa allowances za safari zao.
Wanyonge huwa wananyongwa na wanaonyonga tai
 
Dharau tu naona enzi za jiwe kila mtu aliufyata kuanzia kina Mbowe walikuwa kimya over sudden wote wameota mapembe, ndugai yeye alikuwa anasifia tu kila kitu Hadi vya kijinga
Mfano wa vitu alivyokuwa akisifia ni vipi? Tuache bunge lifanye kazi yake boss
 
Ukweli kwamba walikuwa HAWAKOPI?
Lakini sio kukopa ya kujenga madarasa. Madarasa yalikuwa yakijengwa kwa fedha za michango ya wananchi.
Kwani kuna shida gani ya kujenga kwa michango ya wananchi?
Mikopo ya kuchukua na kupeleka kwenye services ambazo fedha hairudi ni kuruhusu Wakopeshaji wa kimataifa kuchezeq uchumi wetu. Mama aambiwe na alijue hilo.
 
Imefikia hatua Spika anamkosoa kila lililo jema na kukubali yasiyofaa. Ukosoaji wa namna hii si afya kwa ustawi wa nchi yetu.

Tabia hii ameanza kuonesha katika hiki cha awamu ya sita. Mbona Rais Magufuli alikuwa anafanya yanayofanywa na awamu hii lakini hakuwahi kukosoa?

Ukosoaji wa aina ya Ndugai ni moja wa ufa hatari sana katika ukuaji wa uchumi na maendeleo ya nchi. Ukiachana na nchi chache sana duniani ambazo zina uchumi imara wa kujiendesha zenyewe, nchi nyingi zinategemea mikopo ili kukamilisha ujenzi.

Spika licha ya kujua umuhimu wa mikopo yenye riba nafuu na masharti rahisi lakini bado anaona mikopo hiyo haifai. Bila kutoa njia mbadala wa kuongeza mapato ya ndani anapinga mikopo nafuu. Je, maendeleo yatakujaje?

Yawezekana Spika kaona siku zake za kukalia kiti cha uspika zimeisha au ana nia na lengo tofauti la kumkwamisha Rais na Mwenyekiti wake.

Rais na Mwenyekiti wangu, nguvu na uwezo wa kumtoa Spika unao, fanya sasa kabla uharibifu wa Spika haujaota mizizi itakayokuwa migumu kuing'oa
huna akili wewe, hamtaki kuambiwa ukweli, sasa mfukuzeni sppika muone.
 
Serikali tungefikiria kuifanya barabara ya dom high way road leo tusingefikia hatua ya kusemana kisa madeni
 
Miradi kama ya Maji ni huduma ambazo moja kwa moja zinalipiwa kupitia mamlaka za maji za mijini na vijijini. Ni miradi ambayo cash flow yake inajulikana. Kwa hiyo mikopo kama ule wa Arusha wa 520B unajulikana kabisa jinsi mkopo utakavyorudi.
Mikopo kwa ajili ya miradi ya nishati mfano tukikopa kwa ajili ya kuharakisha ujenzi wa bwawa la Julius Nyerere Hydroelectric Power Plant, inaeleweka kabisa jinsi mkopo utakavyorudi kwa sababu ni huduma ya kulipiwa moja kwa moja.
Tukikopa kwa ajili ya kuharakisha ujenzi wa SGR, inajulikana kabisa jinsi flow of cash kwenye hiyo sekta. Hivyo mkopo unajulikana utakavyorudi.
 
Hajatoa njia mbadala ya nini kifanyike? Si kuna tozo?
Mkapa alipingwa na CCM wenzake
Kikwete alipingwa na CCM wenzake akiwemo sitta ndio maana sitta hakurudi awamu ya pili
Magufuli alipingwa na CCM wenzake
Mama Samia anapingwa na CCM wenzake
Hakuna suala la kusema sijui kwa kuwa mwanamke au sijui anaonewa
Acheni ujinga
 
Dharau tu naona enzi za jiwe kila mtu aliufyata kuanzia kina Mbowe walikuwa kimya over sudden wote wameota mapembe, ndugai yeye alikuwa anasifia tu kila kitu Hadi vya kijinga
Sio kweli jiwe alipingwa sana kuanzia ndani ya CCM Hadi nje.
Kusema watu waliufyata ni uongo mkubwa
 
Waliokuwa wakitupeleka vizuri ni awamu ya 5. Ni ngumu kumeza ukweli lakini walikuwa wakituambia ukweli. Uchumi wa kujidanganya kwa mikopo ya hovyo na kutumia hovyo ni kujidanganya ya hali ya juu sana.
Deni la taifa lilikua zaidi kipindi Cha awamu ya 5 sasa unachosifia ni nini? Madudu yote aliyofanya kwa kutengezea propaganda zake na ujingi wa wananchi ndio mtaji wao, acha wale nchi tu
 
Lakini sio kukopa ya kujenga madarasa. Madarasa yalikuwa yakijengwa kwa fedha za michango ya wananchi.
Kwani kuna shida gani ya kujenga kwa michango ya wananchi?
Mikopo ya kuchukua na kupeleka kwenye services ambazo fedha hairudi ni kuruhusu Wakopeshaji wa kimataifa kuchezeq uchumi wetu. Mama aambiwe na alijue hilo.
Nimeshangaa sana watu kushadadia mikopo ya kujenga madarasa...Kweli jamani!
 
Hii kauli ya DENI NI HIMILIVU wasipoachana nayo watakopa mpaka wataweka nchi rehani
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Ndugai anaweza kuzisukuma kete?....hao Msoga Inc wanasukuma kete balaa, muulize EL na ulipo tupo....Ndugai kaa mkao wa kula hao jamaa watalaam wa fitina, jifunze kwa Mzee Six na uwaziri mkuu....
 
Lakini tunavyopotea kuendeleza kukopa kwa ajili ya sekta ya elimu, tunapotea na tunatengeneza mzigo ambao utatutesa sisi ambao bado vijana, utawatesa watoto wetu na vizazi vijavyo. Sekta ya elimu bado ni sekta inayohudumiwa kwa fedha nyingi za walipakodi kupitia elimu bure. Na hiyo ni recurrent expenditure tu maanake haitegemewi kuzalisha flow of cash back to treasury.
Na bado kuna mkopo mwingine ulioitwa mkopo wa "Higher Education Improvement for Economic Transformation"; Terminology ya Benki ya Dunia.
Imeelekezwa kwenye elimu ya juu ambayo nayo bado tunaihudumia kupitia fedha za walipa kodi kupitia mikopo ya elimu ya juu, ruzuku na stahiki mbali mbali za Wafanyakazi wa kada mbali mbali katika ngazi hiyo ya elimu
Bado tena kuna mkopo maarufu kama SEQUIP(Secondary Education Quality Improvement Programme) kwa ajili ya kuboreshea elimu ya sekondari.
Mikopo yote hiyo imetolewa na benki ya dunia kimtego kabisa. Wakijua kabisa kwamba ni pesa ambayo hairudi na hivyo kuisababishia serikali mzigo mkubwa wa madeni. Hivyo serikali kurudi kuwakamua walipa kodi wale wale ili iweze kurejesha mkopo. Na wakati wa kulipa hairudi kwa mipango yake ikiwa imetulia. Inarudi ikiwa na pressure ya kufikia kuitwa International defaulter au isiyokopesheka.
 
Kwa speeda ya samia unaona mikopo yake tutaishia wapi? Af bora vifanyike vitu vya maana kama kumalizia miradi mikubwa eti tunajenga madarasa ambayo yanazalisha majobless baada ya miaka 15
Tusitengeneze job seekers, tuwe na majob creators, sasa mfumo wenyewe wa elimu ndio tabu tupu, kinachotakiwa ni kubadilisha mfumo wote wa elimu ili wasomi wapate ujuzi na sio kutegemea elimu kupata kazi, watu wengi ambao ni wasomi je wanaweza pata ajira wote?
 
Back
Top Bottom