Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 94,296
- 122,540
Katika pita pita zangu kwenye mitaa ya YouTube nimekutana na hii video kutoka ITN Archive yenye mkusanyiko wa matukio ya mambo yaliyojiri baada ya kuuliwa kwa Indira Gandhi, aliyekuwa waziri mkuu wa India, siku ya tarehe 31 Oktoba, 1984.
Siku ya mazishi ya kitaifa, viongozi wengi sana kutoka mataifa mbalimbali walihudhuria, akiwemo Rais wa Tanzania kwa wakati huo, Julius Nyerere na mkewe Maria Nyerere.
Video ni ndefu. Nyerere anaonekana kwenye dakika ya 55:23/24.
Mtangazaji wa ITN alimgundua na kumtaja kwa jina kabisa!
View: https://youtu.be/v7SqLi1VHKA?si=5tBYB8dHEiTyKNZi
Kukosekana kwa vituo vya televisheni kulitunyima sana uhondo wa kuona vile ambavyo viongozi wetu walivyokuwa wanatuwakilisha kimataifa na vile ambavyo Tanzania ilijijengea heshima chini ya Rais Nyerere!
Miaka 10 baadaye, 1994, ndo Tanzania bara ikaja kupata vituo vyake vya televisheni, DTV, CTN, na ITV!