Rais Paul Biya wa Cameroon anasurika kifo Ufaransa akisherekea miaka 40 ya Urais

Biya ni bambeleke?
 
Biya ni bambeleke?
Hapana hawezi kwasababu ndio adui namba moja ya Bambeleke. Paul Biya anawaua sana kwasababu Bambeleke wanachochea sana Cameroon kujitenga.

Cha kushanganza Bambeleke wengi ni kutoka French speaking Franco fone lakini wanataka yale majimbo mawili ya Anglo fone yajitenge.

paul Biya ametoka kabila la Fang. Interestingly hili kabila la Fang pia liko Cameroon, Gabon na equaterial Guinea. Na pia ni kabila la Ali Bongo Rais wa Gabon na Teodoro Obiang wa Equaterial Guinea.
 
Huyo mwamba alishausoma mchezo akisepa anasepa na urais wake hataki ujinga πŸ˜€
Mkuu Paul Biya hata akiwa nje ya nchi hana wasiwasi na urais wake. Kwani kajaza ndugu na kabil
a lake karibia nafasi nyeti serikalini na jeshini. Pia kuna Jeshi lake ndani ya Jeshi la Camroon.

Hao ndugu zake ni wakatili balaa na wanalinda madaraka ya Paul Biya kwa udi na uvumba.

Pili makabila mengine mengi yanamuunga mkono licha ya udikteta ilmradi tu Bambeleke wasipate madaraka.

Tatu Biya ana support ya pekee kutoka Ufaransa, Uingereza na Marekani.

Nilishaletafa uzi kwenye ID yangu ya Maghayo 2020 kuhusu siasa za Cameroon na kabila la Bambeleke.

Jeremy Njitap ni Bambeleke. Na Fan Sam Thomas aliyeimba Danse Danse African collection ni Bambeleke.
 
Biya ni kama CCM tuu, yanashindwa uchaguzi kila mwaka yanabaki kwa kuiba kura tuu na kutumia state organs kulazimisha power, lakini Cameroonians bado wanasumbuliwa sana na ukabila na akili za kikoloni maana bado wanachukiana Francophone na Anglophone, hata akiondoka Biya ukabila bado utawamaliza tuu
 

Huyu na Jezebel wake imetosha sasa. Wee nchi gani watu wanazaliwa mpaka wanakuwa na miaka 40, hawajawahi ona rais mwingine.
 
SAHIHISHO KIDOGO: Rais Paul Biya hakuwa Paris wakati wa kuadhimisha miaka 40 ya utawala wake nchini Cameroon. Bali "Chawa " wake wanaoishi Paris ndiyo waliandaa sherehe hiyo ya kuadhimisha miaka 40 ya Paul Biya kama Rais wa Cameroon. Na waliowafanyia fujo ni wapinzani wa Biya wanaokaa nje ya Cameroon wakiwapo nchi nyingi za Ulaya including France. Siyo kitu chepesi kwa Paul Biya kutokeza hadharani nakukutana na comon men
 
Unapata faida gani na uongo wako
 
Njia pekee ya mabadiriko africa ni kwa njaia ya mapinduzi tu
 
Katumia divide and rule,hayo madudu sijui Anglophone na Francophone yameundwa kuwagawanya Ili wasiungane na kumuondoa huyo Shetani
 
Hapo kwenye ukabila sasa ndio patawatafuna vibaya sana.
 
Duh! Kwenye ukabila tumshukuru JK wa kwanza alicheza kama Zidane 1998 World CupπŸ˜€πŸ˜€
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…