whiteskunk
JF-Expert Member
- Jul 24, 2021
- 3,904
- 9,342
ICC kazi kwao kumkamata, yupo Ukraine anavinjari mitaa ya mauripol
===
Rais wa Urusi Vladimir Putin na Rais pendwa duniani ama mwamba wa dunia jana amefanya ziara ya kushtukiza katika rasi ya Crimea katika kuadhimisha miaka tisa tangu alipoinyakua kutoka Ukraine
Putin aliutembelea pia mji wa Ukraine wa Mariupol unaokaliwa kimabavu huku Mahakama ya wazungu wa ulaya magharibi wakibaki midomo wazi wasijue cha kumfanya.
Ziara ya Putin inajiri siku chache baada ya Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu ICC kutoa waranti wa kukamatwa kwake kwa uhalifu wa kivita, ikimtuhumu kwa uwajibikaji katika utekaji nyara wa watoto nchini Ukraine.
Moscow imetupilia mbali uamuzi wa Mahakama hiyo. Kyiv inasema tangu kuanza kwa uvamizi huo Februari 2022, zaidi ya watoto 16,000 wa Ukraine walihamishwa kinyume cha sheria kuelekea Urusi. Wakati huo huo, mapigano makali yanaendelea huko Donetsk hasa katika mji wa Bakhmut.