Hapo nadhani wanailump Afrika lakini kama wangekuwa specific wangesema Afrika Kaskazini, Somalia, Ethiopia, Sudani Kusini, na baadhi ya nchi za West Africa ndiko wanahitaji hiyo ngano ya Russia.
Hata hivyo kuna namna fulani hivi ambavyo mwafrika akili yake ni ndogo sana. Udogo wa akili ya mwafrika ni jinsi ambavyo wazungu wanavyoweza kutengeneza tatizo, wakalibrand kuwa ni tatizo kubwa kwa mwafrika, na mwafrika akaibeba mazima mazima hiyo simulizi ya mzungu na kuliona kuwa ni tatizo kwake. Mwisho ni mwafrika kuendelea kuwa tegemezi kwa mzungu milele na milele.
Mfano mdogo ni kuhusu corona. Corona ilivyoanza huko Ulaya na Marekani wakawa wakifa kama kumbikumbi yet simulizi kwenye vyombo vya habari vya wazungu ilikuwa ni jinsi ambavyo Afrika itakuwa "disproportionately hit" na corona. Wakati huo nafikiri Afrika ilikuwa hata haijapata hata mgonjwa mmoja wa corona. Lakini viongozi wa AU save Tanzania walivokuwa busy kujigonga gonga na kulialia kwa mataifa ya Ulaya na Marekani kuhusu chanjo, na jinsi mataifa hayo yanavyokumbatia chanjo utafikiri basi waafrika ndio tunaihitaji chanjo kuzidi wao. Ni akili ndogo tu na utumwa utumwa tu.
Na hata kwenye hii ishu ya Russia na Ukraine na madhara yake kiuchumi. Kama kuna madhara Afrika itayapata kutokana na hii vita hatutakuwa tofauti na watu wa mabara mengine. Huyo Sall kukimbilia Russia kuomba sijui hiki au kile ni utoto utoto tu wa viongozi wa kiafrika.