Rais Putin kutangaza usiku huu Russia kutambua rasmi majimbo huru yaliyojitenga ya Donetski na Luhansk


He has beaten them again tactically! Putin is a smart spy. He knows how to play the game. Hapo ngoma imeanza
 
Wasituletee vita ya 3 ya dunia kwa sababu ya upumbavu wao. Maana vita ya 3 kwa technolojia iliyopo wote tutakwisha including wao. Washenzi hawa wananibore sana.
Mkuu wachukulie poa tu! Hakuna vita ya 3 ya dunia.
 
Sasa hayo majimbo inamaana yamemeguka toka russia au

Toka Ukraine, yanakuwa sehemu ya washirika wa Russia. Hivyo Russia itapinga aina yoyote ya uvamizi wa kijeshi maeneo hayo.

Kumbuka UN inatambua haki ya watu kujitambua kuwa huru hapo wamecheza na saikolojia wa Ukraine. Kwamba majimbo hayo yanataka kujitenga na Ukraine.

Russia itatuma majeshi yake kuwasaidia shughuli ya kutimua majeshi ya Ukraine na NATO wakijichanganya ndo vita hivyo.
 
EU wanatakiwa wakatae kucheza ngoma ya USA .USA alipoitambua Jerusalem kama makao makuu ya Israel why hawakumfanyia sanctions ?Russia na USA wanabore sana.
Umeanza kubadilika kidogokido,najua Shemeji anafanya kazi yake vizuri ya kukuelimisha.
Inabidi ujue Sasa kuwa chokochoko zote hizi ni US,ndio anataka kuizunguka kijeshi Russia.
Marekani anakaa mbali huko NATO ya Nini?
Sasa Russia wale ni akili nyingi hawaruhusu Adui yake USA amsogelee kupitia mgongo wa NATO.
Utaelewa taratibu TU,hata Mimi nilikua kama wewe.
Ila kwa mambo ya CCM aisee uko juu.
Maana ulikua unatupa Up date sahihi kabisa za hali ya afya ya yule aliekua anatamani kuja kuwa Mkuu wa malaika.
 
Sijawahi badilika. Binafsi sina upande. Huwa ninaanalyse kila mmoja wao mazuri na mabaya yake.
 
Kuhusu Nato nilimponda USA.Leo nimemponda Putin kwa kutambua sehemu ya Ukraine ambao ni pro Russia kama sehemu huru.Mimi sina upande. Ukitaka ujadili vizuri hawa mataifa wawili ni vyema kutokuwa na upande maana wote ni wapumbavu.
 

Katika dunia ya leo, nchi inayojivunia silaha kubwa huku uchumi unazidi kudumaa haina cha kujivunia.

Russia tangu enzi za USSR imekuwa ikirudi nyuma kiuchumi kiasi cha kukaribia dunia ya tatu na kutegemea mikopo ya IMF na WB. Bado uchumi wake unategemea sana mauzo ya malighafi ya mafuta (petroleum na natural gas) kuliko bidhaa za teknolojia.

Wanaimarisha silaha kama North Korea huku idadi ya watu wanaoishi kiujima ikiongezeka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…