Rais Putin kutangaza usiku huu Russia kutambua rasmi majimbo huru yaliyojitenga ya Donetski na Luhansk

Rais Putin kutangaza usiku huu Russia kutambua rasmi majimbo huru yaliyojitenga ya Donetski na Luhansk

IMG_2349.jpg
 
View attachment 2126631
Raisi Vladimir Putin akitia saini amri (the Decree) kutambua majimbo ya Donestk na Luhansk kuwa majimbo huru. Picha na Reuters.

Raisi wa Russia Vladimir Putin usiku huu anatarajiwa kutangaza majimbo ya Donetsk na Luhansk kama majimbo huru.

Majimbo haya mawili yaliyo upande wa mashariki mwa Russia, ndio kiini cha mzozo unoendelea unaozihusu nchi za Ukraine, NATO, Russia, Marekani na nchi za magharibi.

Pia raisi Putin atasaini amri (decree) ya kutambua eneo zima lijulikanalo kama Donbass kama eneo la Russia.

Baada ya kutangaza uamuzi huo wa Russia, kiongozi huyo wa Russia ataamuru majeshi ya Russia kuingia katika majimbo hayo ili kulinda maslahi ya Russia kiusalama na kijeshi.

Raisi wa Ufaransa Emmanuel Macron ameitisha kikaao cha dharura cha umoja wa mataifa ambapo suala la uamuzi wa Russia kutambua majimbo ya Donetski na Luhansk litajadiliwa.

Wakati huohuo Russia imeitisha kikao cha dharura umoja wa mataifa kujadili suala la Ukraine baada ya mkuu wa majeshi ya Russia kusema kwamba Ukraine imeweka majeshi yapatayo 60,000 katika eneo la Donbass.

Putin anadai kwamba kiongozi wa ilokuwa USSR Lenin alifanya maamuzi ya kimakosa katika kuangalia mipaka ya USSR na ndio kiini cha matatizo ya leo hii.

He has beaten them again tactically! Putin is a smart spy. He knows how to play the game. Hapo ngoma imeanza
 
Wasituletee vita ya 3 ya dunia kwa sababu ya upumbavu wao. Maana vita ya 3 kwa technolojia iliyopo wote tutakwisha including wao. Washenzi hawa wananibore sana.
Mkuu wachukulie poa tu! Hakuna vita ya 3 ya dunia.
 
Sasa hayo majimbo inamaana yamemeguka toka russia au

Toka Ukraine, yanakuwa sehemu ya washirika wa Russia. Hivyo Russia itapinga aina yoyote ya uvamizi wa kijeshi maeneo hayo.

Kumbuka UN inatambua haki ya watu kujitambua kuwa huru hapo wamecheza na saikolojia wa Ukraine. Kwamba majimbo hayo yanataka kujitenga na Ukraine.

Russia itatuma majeshi yake kuwasaidia shughuli ya kutimua majeshi ya Ukraine na NATO wakijichanganya ndo vita hivyo.
 
EU wanatakiwa wakatae kucheza ngoma ya USA .USA alipoitambua Jerusalem kama makao makuu ya Israel why hawakumfanyia sanctions ?Russia na USA wanabore sana.
Umeanza kubadilika kidogokido,najua Shemeji anafanya kazi yake vizuri ya kukuelimisha.
Inabidi ujue Sasa kuwa chokochoko zote hizi ni US,ndio anataka kuizunguka kijeshi Russia.
Marekani anakaa mbali huko NATO ya Nini?
Sasa Russia wale ni akili nyingi hawaruhusu Adui yake USA amsogelee kupitia mgongo wa NATO.
Utaelewa taratibu TU,hata Mimi nilikua kama wewe.
Ila kwa mambo ya CCM aisee uko juu.
Maana ulikua unatupa Up date sahihi kabisa za hali ya afya ya yule aliekua anatamani kuja kuwa Mkuu wa malaika.
 
Sijawahi badilika. Binafsi sina upande. Huwa ninaanalyse kila mmoja wao mazuri na mabaya yake.
 
Umeanza kubadilika kidogokido,najua Shemeji anafanya kazi yake vizuri ya kukuelimisha.
Inabidi ujue Sasa kuwa chokochoko zote hizi ni US,ndio anataka kuizunguka kijeshi Russia.
Marekani anakaa mbali huko NATO ya Nini?
Sasa Russia wale ni akili nyingi hawaruhusu Adui yake USA amsogelee kupitia mgongo wa NATO.
Utaelewa taratibu TU,hata Mimi nilikua kama wewe.
Ila kwa mambo ya CCM aisee uko juu.
Maana ulikua unatupa Up date sahihi kabisa za hali ya afya ya yule aliekua anatamani kuja kuwa Mkuu wa malaika.
Kuhusu Nato nilimponda USA.Leo nimemponda Putin kwa kutambua sehemu ya Ukraine ambao ni pro Russia kama sehemu huru.Mimi sina upande. Ukitaka ujadili vizuri hawa mataifa wawili ni vyema kutokuwa na upande maana wote ni wapumbavu.
 
Wanaomu underate russia wakasome dude linaitwa tsar bomber au the weapon of last resort ndio bomu kubwa la nyuklia kuwahi kutengenezwa dunia haijapata tokea mpaka leo na toka kuumbwa kwa ulimwengu na hiyo ni mwaka 1961 wakati cc ndio tunapata uhuru sasa jiulize huyu mtu leo atakuwa wapi?

Katika dunia ya leo, nchi inayojivunia silaha kubwa huku uchumi unazidi kudumaa haina cha kujivunia.

Russia tangu enzi za USSR imekuwa ikirudi nyuma kiuchumi kiasi cha kukaribia dunia ya tatu na kutegemea mikopo ya IMF na WB. Bado uchumi wake unategemea sana mauzo ya malighafi ya mafuta (petroleum na natural gas) kuliko bidhaa za teknolojia.

Wanaimarisha silaha kama North Korea huku idadi ya watu wanaoishi kiujima ikiongezeka.
 
Back
Top Bottom