Rais Rajapaksa wa Sri Lanka huenda akakimbia nchi

Rais Rajapaksa wa Sri Lanka huenda akakimbia nchi

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Rais wa Sri Lanka ambaye anatarajiwa kukabidhi madaraka Julai 13, 2022, Gotabaya Rajapaksa inadaiwa alipelekwa katika kambi ya jeshi la wanaanga karibu na uwanja mkubwa wa ndege wa kimataifa.

Hayo yameelezwa na maafisa nchini humo wakati zikiongezeka fununu kwamba ataikimbia nchi na kwenda uhamishoni ng'ambo.

Afisa mwandamizi katika wizara ya ulinzi amesema kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 73 alikimbilia kwanza katika kambi ya jeshi la wanamaji kabla ya kupelekwa katika kambi ya jeshi la wanaanga ya Katunayake iliyoko karibu na uwanja mkuu wa ndege wa Sri-Lanka.

Mpaka sasa hakuna taarifa rasmi kuhusu aliko rais huyo ingawa vyombo mbali mbali vya habari nchini Sri-Lanka vimeripoti kuhusu tetesi kwamba anajiandaa kuelekea Dubai leo jioni.Kiongozi mkuu wa upinzani Sajith Premadasa kwa uapnde mwingine amesema wako tayari kuunda serikali.'Bunge litamchagua rais Julai 20.

Pesa taslimu, rupee milioni 17.85 ambazo ni sawa na kiasi dola elfu 50 zilizoachwa na rais Rajapaksa katika makaazi yake zimekabidhiwa mahakama hii leo na waandamanaji.
===

Sri Lanka President Flown To Airbase As Exile Rumours Spread: Report

Sri Lanka's embattled president was flown to an airbase near the main international airport Monday, officials said, raising speculation he will flee into exile abroad.

Gotabaya Rajapaksa fled the presidential palace in Colombo under naval protection on Saturday, shortly before tens of thousands of protesters overran the compound.

Hours later, the parliamentary speaker announced Rajapaksa would resign on Wednesday to allow a "peaceful transition of power".

The 73-year-old leader had taken refuge at a navy facility, a top defence official told AFP, before being brought to the Katunayake airbase -- which shares a perimeter fence with the country's main Bandaranaike International airport.

"He and his entourage were flown back to Colombo in two Bell 412 choppers," he added.

There was no official word from the president's office about his whereabouts, but several local media reports speculated he was set to leave for Dubai later Monday.

Prime Minister Ranil Wickremesinghe's office said Rajapaksa had officially informed him of his intention to resign, without specifying a date.

Source: Ndtv
 
Usishangae akakimbilia marekani au ulaya kwa hao wazungu ambao kutwa tunawasimanga .
 
Usishangae akakimbilia marekani au ulaya kwa hao wazungu ambao kutwa tunawasimanga .
si unajua hizo nchi NI sawa na dumpo mkuu, inapokea kila kitu mkuu.kwingine huko Kama una walakini ,hawakupokei kizembe zembe .
 
😁😁😁
image32.jpg
 
Back
Top Bottom