Uko sahihi kwa yote. Lakini kuna eneo aidha sijakuelewa vyema au hujaeleweka vyema. State Funeral hupewa mtu ambaye mchango wake wa kitaifa umeleta Mapinduzi na mchango wa Kipekee ambao hata watu wengine kwenye sekta hiyo wanaafiki; na kazi hiyo imekuwa na mchango wa kutambulika kwa jamii husika. Madilu, Pepe Kalle hao walikuwa ni wasanii wakubwa, lakini Hawakufikia Franco. Franco aliubadili muziki, kuukuza na kuutambulisha nje kwa miaka karibu 30 na hatimaye kuitwa mfalme wa Rhumba. Lakini, sifa nyingine ni ushawishi wa mtu huyo kwa jamii. Baada ya kuwa ametambulika sana kwa kazi yake na heshima aliyoijenga, basi jamii inamsikiliza na kuweza kufuata ayasemayo—USHAWISHI. Sasa mtu kama Franco alikuwa na uwezo wa kusimama na kusema mchagueni fulani na watu wakachagua. Pia kuna wanamuziki kama Umm Khulthum. huyu wamisri walikuwa wakimtazama kama alama ya taifa lao. Kuna wakati Rais Gamal El Nasser alikuwa hawezi ongea watu wakamuelewa hadi huyu mama azungumze. Alipofariki karibu Robo ya watu wa Misri waliingia barabarani kwenye msururu wa mazishi yake, alipewa hadhi ya kuwa Balozi (Diplomatic Status). Wanamuziki/wasanii wa kaliba hii ndio hupewa hadhi ya mazishi ya kitaifa. Sasa wampime AKA kama anaweza kufika hadhi hiyo, au ni watu kama kina Yvyone Chaka Chaka kwa Afrika kusini ndio wanaweza kufikiliwa. Je, Diamond ana hadhi hiyo. Diamond amekuta Bongo Flava imeshaanza wala hakuna mapinduzi aliyoyafanya kwenye muziki zaidi ya kujisimamia yeye binafsi na kuwa model ya namna ya kuendesha biashara ya muziki wa bongo flava (kwa hili anastahili heshima). Lakini hapa inabidi tufanye tafakari. Waasisi wa bongo flava ni watu wanaopaswa kuwa na hadhi ya kutambuliwa kutokana na kitu walichokileta kwenye jamii—watambulike Kiserikali na kitaifa—changamoto hapa ni moja, nani anasifa ya kuwa Icon wa Bongo flava.