Rais Ramaphosa akataa Rapa AKA kufanyiwa mazishi ya Kitaifa

International Arts wana mchango mkubwa kwa mataifa yao, kwa mfano, Muziki wa Congo umefika hapo ulipo leo sababu ya watu kama Franco ndio maana alipewa state funeral, wanamuziki wana mchango Mkubwa kwa Taifa kuliko wanasiasa wengi

Hapo Tanzania leo, Diamond ana mchango mkubwa kwa Taifa kuliko kina Nape na Mwigulu
Sio kila mwanamziki anafikia hadhi hiyo!!kwa DRC mbona ni wengi wamefariki lakini ni FRANCO pekee ndiye epewa heshima hiyo?ni ukweli usiopingika kwa mziki wa congo aliufanyia kazi kubwa sana!!
Hata kama diamond ana mchango huo lakini hajafikia sifa hiyo ya kuzikwa kitaifa kama akifa.
 
Uko sahihi kwa yote. Lakini kuna eneo aidha sijakuelewa vyema au hujaeleweka vyema.

State Funeral hupewa mtu ambaye mchango wake wa kitaifa umeleta Mapinduzi na mchango wa Kipekee ambao hata watu wengine kwenye sekta hiyo wanaafiki; na kazi hiyo imekuwa na mchango wa kutambulika kwa jamii husika.

Madilu, Pepe Kalle hao walikuwa ni wasanii wakubwa, lakini Hawakufikia Franco. Franco aliubadili muziki, kuukuza na kuutambulisha nje kwa miaka karibu 30 na hatimaye kuitwa mfalme wa Rhumba. Lakini, sifa nyingine ni ushawishi wa mtu huyo kwa jamii. Baada ya kuwa ametambulika sana kwa kazi yake na heshima aliyoijenga, basi jamii inamsikiliza na kuweza kufuata ayasemayo—USHAWISHI.

Sasa mtu kama Franco alikuwa na uwezo wa kusimama na kusema mchagueni fulani na watu wakachagua. Pia kuna wanamuziki kama Umm Khulthum. huyu wamisri walikuwa wakimtazama kama alama ya taifa lao. Kuna wakati Rais Gamal El Nasser alikuwa hawezi ongea watu wakamuelewa hadi huyu mama azungumze. Alipofariki karibu Robo ya watu wa Misri waliingia barabarani kwenye msururu wa mazishi yake, alipewa hadhi ya kuwa Balozi (Diplomatic Status). Wanamuziki/wasanii wa kaliba hii ndio hupewa hadhi ya mazishi ya kitaifa.

Sasa wampime AKA kama anaweza kufika hadhi hiyo, au ni watu kama kina Yvyone Chaka Chaka kwa Afrika kusini ndio wanaweza kufikiliwa. Je, Diamond ana hadhi hiyo. Diamond amekuta Bongo Flava imeshaanza wala hakuna mapinduzi aliyoyafanya kwenye muziki zaidi ya kujisimamia yeye binafsi na kuwa model ya namna ya kuendesha biashara ya muziki wa bongo flava (kwa hili anastahili heshima).

Lakini hapa inabidi tufanye tafakari. Waasisi wa bongo flava ni watu wanaopaswa kuwa na hadhi ya kutambuliwa kutokana na kitu walichokileta kwenye jamii—watambulike Kiserikali na kitaifa—changamoto hapa ni moja, nani anasifa ya kuwa Icon wa Bongo flava.
Acha ubishii jombaa, wasanii wote wanamichango mikubwa kwa mataifa yao.

Moja wapo[emoji117], huduma ya burudani kwa wananchi haijalishi maudhui yanayotumika, lkn kinanchoangaliwa ni ushawishi wake kwa raia kama wamependezwa na huduma hiyo ya muziki, akiimba matusi na raia wakafurahia basi hiyo huduma imekubalika na jamii yake.

Namba mbili[emoji117] kwa mfano wa diamond huyu akifa sio kufanyiwa mazishi ya kitaifa tu bali sanamu yake ijengwe makao makuu ya nchi, kwa sababu gan? Kama wew si mfuatiliaji wa muziki wa bongo huwezi kuelewa utabaki kubisha bisha,

Huyo kijana diamond kaikuta tasnia ya muziki wa bongo ikiwa ya hovyo, tasnia iliyotoa mastaa wenye majina makubwa kuliko hali zao za kiuchumi.

Amekuwa msanii wa kwanza kuitambulisha Tanzania kimataifa na msanii wa kwanza kubeba Tuzo ambazo hakuna pimbi amewai kuzibeba Tanzania tangu dunia inaumbwa,

Pia msanii wa kwanza kuajiri vijana wengi na kuchangia kodi kubwa kwa taifa zaidi ya 1bilion anachangia kwa Taifa kila mwaka, na ushahidi upo, je mbunge wako anachangia kiasi gani?

Pia kuifanya tasnia ya muziki kuwa biashara yenye faida kwa kubadiri aina ya muziki, style na connection ya kazi za kisanaa
msanii wa kwanza Tanzania kwa ushawishi kwa vijana kujiunga na tasnia ya muziki bila kusahau kuipa heshima tasnia hii nje na ndani ya nchi, kawaulize Kenya, Ug, Nigeria,

Acheni chuki kwa wasanii, mnajifanya wapenda maudhui mazuri lkn tabia zenu huko mafichoni ni chafu kulko hata hao wasanii.

Afrika kusini ni moja ya nchi za kipuuzi sana, ingekuwa nchi nyingine basi msanii huyo AKA alipaswa heshima ya mazishi ya kitaifa,

Jifunzeni kwa beberu wenu USA na washirika wake wa magharibi wanavyojua kuwajali wasanii wao ndiomaana hata kazi za sanaa nchi hizo zinaheshimika kuliko hivi vinchi mnavyojifanya mnayajua maadili sana kumbe mmejawa uchafu wa kila aina.
 
International Arts wana mchango mkubwa kwa mataifa yao, kwa mfano, Muziki wa Congo umefika hapo ulipo leo sababu ya watu kama Franco ndio maana alipewa state funeral, wanamuziki wana mchango Mkubwa kwa Taifa kuliko wanasiasa wengi

Hapo Tanzania leo, Diamond ana mchango mkubwa kwa Taifa kuliko kina Nape na Mwigulu
"International Arts", sasa hii ndiyo nini! Lugha kama hauijui iache ikupitilie mbali, hata jiwe alilijua hilo.
 
Unachosema wasanii wote wanatakiwa kupata mazishi yenye hadhi ya kitaifa?
 
International Arts wana mchango mkubwa kwa mataifa yao, kwa mfano, Muziki wa Congo umefika hapo ulipo leo sababu ya watu kama Franco ndio maana alipewa state funeral, wanamuziki wana mchango Mkubwa kwa Taifa kuliko wanasiasa wengi

Hapo Tanzania leo, Diamond ana mchango mkubwa kwa Taifa kuliko kina Nape na Mwigulu
Diamond anafaida gani Kwa Taifa?
 
South Africa sio Taifa la kisanaa , kuna mataifa Sanaa ni nembo ya Taifa Lao , hlo ni Taifa la kisiasa Zaid , mfano hyo Congo ni Sawa , Argentina au Brazil Kwa mpira ni Sawa , Ila South Africa Kwa kuimba tuu , big noo
Ila Lucky Dube (Rip) aliwawakilisha vyema enzi hizo.
 
Back
Top Bottom