Rais Ruto aagiza Polisi kuwapiga risasi za Miguuni Waandamanaji wanaoharibu biashara za watu

Rais Ruto aagiza Polisi kuwapiga risasi za Miguuni Waandamanaji wanaoharibu biashara za watu

ChoiceVariable

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2017
Posts
83,659
Reaction score
90,151
Rais wa Kenya William Ruto, akiwa katika hafla ya uzinduzi wa makazi ya polisi eneo la Kilimani, Nairobi, tarehe 9 Julai 2025, alitoa agizo kwa polisi kuwakabili watu wanaohusika na uharibifu wa mali wakati wa maandamano.

Katika hafla hiyo Rais Ruto alisikika akisema

“Wale wanaochoma mali ya wananchi, siyo kuwaua… wapigwe risasi kwa mguu, waende hospitali halafu waende kortini.”

Aidha Rais Ruto Akaongeza:

“Hatutaruhusu watu wachache wachome mali, waibe, waharibu vitu vya wananchi na waseme ni haki yao. Hakuna haki ya kuharibu mali ya mwingine.” Alisisitiza Ruto.

Kauli hiyo inatolewa kufuatia maandamano makubwa yaliyotokea nchini Kenya kuanzia 25 Juni 2025, hasa kupinga Mswada wa Fedha (Finance Bill), hali ngumu ya kiuchumi, na gharama ya juu ya maisha.

Katika maandamano hayo.
  • Vituo vya polisi vilishambuliwa.
  • Mali ya umma na binafsi iliharibiwa.
  • Viongozi wa maandamano walihojiwa, wengine kukamatwa.




1752064520402.png

===
My Take
Hotuba ya Ruto inanikumbusha hotuba ya Rais Samia alivyowaambia Chadomo kwamba Rais haondolewi hivyo 😆😆

Na huku Bongo wale wanaotaka Kuvuruga Uchaguzi Wasichekewe.

Tuna Nchi Moja tuu hatuna pa kukimbilia wao wanalishwa na Mabeberu.

View: https://www.instagram.com/p/DL4c7FPiW6a/?igsh=MWoxZ2l6YzloeWV6bA==
 
Huyu si alisema wao wana police 'service' na sio police 'force'. Sasa hayo ya kupigana risasi yanatoka wapi au ndo huduma zenyewe!
Endelea kuwaamini Wanasiasa wakiwemo hao Chadomo wenu.
 
Inasemekana Ruto na wenzie wametengeneza kikundi cha vijana ambacho katikati ya hizi purukushani kinazunguka kufanya uharibifu wa mali, wizi n.k

Leo kuonesha waandamanaji ni wahalifu tuu.

Inasemekana.
 
Inasemekana Ruto na wenzie wametengeneza kikundi cha vijana ambacho katikati ya hizi purukushani kinazunguka kufanya uharibifu wa mali, wizi n.k

Leo kuonesha waandamanaji ni wahalifu tuu.

Inasemekana.
Ili iwe nini?
 
Kwa nini isivumilike wakati ni Demokrasia? 😂😂
😀 😀 hakuna demokrasia isiyo na mipaka. Katiba ya Kenya ni ya kipuuzi sana. Imewabana mno askari ndo maana nao wameachia tu mambo yaende yanavyoenda. Haina tofauti na rasimu ya Warioba yenye kifungu kinachotaka wananchi wamtoe madarakani mbunge wakiona hafanyi kazi vizuri. Ina maana kutakuwa na chaguzi za mara kwa mara baada ya watu kupigana fitina.
 
Sasa ukisharuhusu hilo ujue kuwa kuna abuse of mamlaka uliyowapa!

Genz na nyiny acheni vurugu, andamana kwa ustaarabu kupata haki zenu au nenda MAUMAU ya pili ijulikane kuwa kuna vita ya kumuondoa Ruto na si kuiba mali za watu
 
Back
Top Bottom