Rais wa Kenya William Ruto, akiwa katika hafla ya uzinduzi wa makazi ya polisi eneo la Kilimani, Nairobi, tarehe 9 Julai 2025, alitoa agizo kwa polisi kuwakabili watu wanaohusika na uharibifu wa mali wakati wa maandamano.
Katika hafla hiyo Rais Ruto alisikika akisema
βWale wanaochoma mali ya wananchi, siyo kuwauaβ¦ wapigwe risasi kwa mguu, waende hospitali halafu waende kortini.β
Aidha Rais Ruto Akaongeza:
βHatutaruhusu watu wachache wachome mali, waibe, waharibu vitu vya wananchi na waseme ni haki yao. Hakuna haki ya kuharibu mali ya mwingine.β Alisisitiza Ruto.
Kauli hiyo inatolewa kufuatia maandamano makubwa yaliyotokea nchini Kenya kuanzia 25 Juni 2025, hasa kupinga Mswada wa Fedha (Finance Bill), hali ngumu ya kiuchumi, na gharama ya juu ya maisha.
Katika maandamano hayo.
- Vituo vya polisi vilishambuliwa.
- Mali ya umma na binafsi iliharibiwa.
- Viongozi wa maandamano walihojiwa, wengine kukamatwa.
===
My Take
Hotuba ya Ruto inanikumbusha hotuba ya Rais Samia alivyowaambia Chadomo kwamba Rais haondolewi hivyo ππ
Na huku Bongo wale wanaotaka Kuvuruga Uchaguzi Wasichekewe.
Tuna Nchi Moja tuu hatuna pa kukimbilia wao wanalishwa na Mabeberu.
View: https://www.instagram.com/p/DL4c7FPiW6a/?igsh=MWoxZ2l6YzloeWV6bA==