William Ruto ni mwanasiasa wa Kenya ambaye amekuwa
Rais wa tano wa taifa hilo kuanzia tarehe 15 Septemba, 2022. Kwa
mujibu katiba ya Kenya Rais anaruhusiwa kuchaguliwa kwa vipindi viwili vya miaka mitano mitano.
Madai
Kipo
kipande cha video kinachomuonesha Rais Ruto akisema
"As the President i will be at the front to change term limit." (“Kama Rais nitakuwa mstari wa mbele kubadilisha ukomo wa muhula.”) huku zikisikika sauti za watu wakishangilia kwa kupiga makofi.
Uhalisia
Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck kwa kutumia Google Reverse Image Search umebaini video halisi iliyochapishwa Novemba 16, 2022 na kituo cha televisheni cha
NTV Kenya kupitia mtandao wa YouTube.
Aidha kupitia marejeo ya video imebainika kuwa kipande hicho cha video kimepotoshwa uhalisia wake kwa kukata na kuunganisha vipande vidogo visivyohusiana hatimaye kupotosha uhalisia.
Akizungumza Ikulu ya Kenya Novemba 16, 2022 Rais Ruto alisisitiza kuwa atakuwa mstari wa mbele katika kuzuia mabadiliko yoyote ya kikatiba kubadili ukomo wa mihula ili kunufaisha watu binafsi.
"Kama Rais, sitashiriki katika kuichakachua Katiba kwa ajili ya kutumikia maslahi binafsi, na yenye upendeleo. Nitakuwa mstari wa mbele kusema hapana kwa mabadiliko yoyote ya katiba, kubadilisha kikomo cha mihula, au kubadili mambo yanayowanufaisha watu binafsi. Hayo hayana ulazima, hayana sababu, na ni zoezi la bure, kwa sababu hayatatokea chini ya uongozi wangu.”
(As president, I will not participate in mutilating the Constitution for purposes of serving selfish, personal, parochial interests, I will be at the front to say no to any change of the constitution, to change the term limit, to change things that benefit individuals. That is unnecessary, that is uncalled for, and it is an exercise in futility, because it will not happen under my watch.”)
View: https://youtu.be/-tWG_V08wYg?si=UPKBX7UbGdDe9Cen