Rais Ruto anasema Congo, Sudan Kusini, Somalia na Haiti wanaitegemea Kenya

Wanyama ndio wamebarikiwa kila kitu kwetu
Sisi tunashindwa hata nyuki tutaweza kushindana na binadamu?

Wao kenya wameanza kilimo cha umwagiliaji miaka mingi sana iliyopita ndio maana mbogamboga nyingi na matunda zinaenda kila mahali
Chai yao mpaka supermarkets za Ulaya zimejaa
Sisi hata packaging πŸ“¦ tu Kikwete alituma vijana kwenda kujifunza Kenya, ni aibu iliyoje?

Rasilimali hizo mlizonazo, mapori yamekaa tu yanaota nyasi badala ya chakula cha kupeleka nje
Kweli akili zetu tunazijua wenyewe
Na tusilaumu mtu wala mfumo bali ni sisi wenyewe

Tupige makofi kwa ujinga
 
Ushahidi ni wewe unitajie nini Tanzania Hatuna πŸ˜„
 
Fikiria familia ya mkulima mwenye wake 4, watoto 30 halafu ana choroko kilo 20, maharage kilo 50, mahindi kilo 1000, dengu kilo 10, kunde kilo 30 (Tanzania).

Halafu kuna familia jirani yako ina mke 1, watoto 3. Lakini ina maharage kilo 5,000 na mpunga kilo 10,000 (Botswana).

Kati ya hawa wawili, familia ipi ina hali bora zaidi?
 
Ruto anaongelea leo halaf wewe unaongelea mambo ya miaka 2100?

Hapo ndipo tuonekanapo wajinga
 
Ninavyofahamu Tanzania ndio nchi iliyobarikiwa kila aina ya Rasilimali hapa duniani na tunategemewa na nchi mbalimbali

Taja nchi zinazoitegema TZ?

Nini TZ inazalisha ambacho nchi zingine hawana? Ni resource gani mnayo au mnaongoza kwa reserve ambayo dunia inaitegemea?

Mafuta, gas, madini, kilimo, mifugo, ardhi, maji, vyote hamuongozi wala kutegemewa, ni nini mnachotegemewa?

Huu uongo mlijazwa kufunga akili zenu and y'all fell for it. Mnajiona special in reality hamna uspecial wowote ule. Mpiga mwingi asingekua anazurura duniani kuinadi Tanganyika kama mngekuwa mnategemewa.

TZ inaongoza kuzalisha wajinga tu.
 
kiswahili chao uwa kina mashaka .maranyingi wanavo jieleza unaweza kujua wanajua
icho kiswahili chao na ndio wanaongoza kuchukua wazungu kuwafundisha kupitia mtandaoni.
Penye ukweli tuseme kenya wametuzidi tatizo tunapenda unafki. Kila siku tunalalalmika Halafu mkisikia mnasemwa mnajifanya hakuna shida.
Kenya sahiv wamembatiza raisi ni tourist president hostess.
Tatizo Watanzania tuna unafki mwingi
 
Acha kupotosha ewe mnafiki. Kasema kuhusu Usalama na sio rasilimali.
 
Aiseeh! Wewe unaongelea miaka mia moja ijayo?.
 
Mgawanyo wa hizo rasilimali ukoje? Wanao bahatika kuzipata mfumo wake ukoje
 
Ruto is no better anasafiri kuliko mpiga mwingi.
 
Ukiangalia kwa upande huo utasema ni bora mwenye familia ndogo
Laikini kuna wenye familia kubwa na wanafanya vizuri kwa kusaidiana na kuwa wamoja
Mkuu Bongo tatizo hakuna umoja
Hawajui partnerships kwa sababu hakuna aliewafundisha kwa elimu au kutokuaminiana
Haiwezekani ukapambana na ukatoboa kwa shamba kubwa peke yako au biashara peke yako huku una familia mpaka shangazi unataka umlishe wewe
Lazima kujifunza kuaminiana na kuwa na malengo na mipango ya miaka hata kumi kwa kusaidiana na kuweka hela pamoja na kufanya kitu cha maana

Mataifa mengi sana wanafanya hivyo, mimi ni sleep partner na ninapata faida kila mwezi sehemu kwa sababu tuna uaminifu na kiwanda kipo nchi tofauti

Mswahili analia tu na anasema bila ndagu hutoboi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…