Rais Ruto anasurika kuvamiwa na kijana wakati akihutubia kongamano la kibiashara la NYOTA Business Forum

Rais Ruto anasurika kuvamiwa na kijana wakati akihutubia kongamano la kibiashara la NYOTA Business Forum

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Maafisa wa usalama wa Rais wa Kenya, William Ruto, wamelazimika kuingilia kati kuzuia kijana mmoja aliyetaka kulisogelea jukwaa wakati Rais akiwahutubia washiriki wa kongamano la kibiashara la NYOTA Business Forum.

Tukio hilo limetokea wakati wa hafla ya kutoa mitaji kwa wafanyabiashara wapya (start-ups), ambapo maafisa walimnasa mwanamume huyo kwa haraka kabla ya kufika jukwaani na kumdhibiti. Baada ya hali ya utulivu kurejea, Rais Ruto alitoa maelekezo kwa timu yake ya ulinzi kumshikilia mwanamume huyo kwa muda, akiahidi kushughulikia jambo lake baadaye.

Mradi wa NYOTA (National Youth Opportunities Towards Advancement) ni programu ya Serikali inayolenga kutoa fursa kwa vijana na kuwawezesha kiuchumi. Mradi huu ni sehemu muhimu ya Ajenda ya Rais Ruto ya Maendeleo ya Kiuchumi kutoka Chini Kwenda Juu (BETA - Bottom-Up Economic Transformation Agenda), inayokusudia kuwapa vijana ujuzi wa kibiashara na mitaji, kuupanua fursa za ujasiriamali kwa kutoa mitaji ya kuanzia (start-up capital) na kutengeneza njia rasmi za vijana kujipatia kipato cha kudumu.

 
Back
Top Bottom