Rais Samia aagiza Darasa la Saba waliofutwa kazi walipwe stahiki zao

Huyu lazima atakuwa mhanga wa vyeti feki....yaani

Sijaelewa mantiki ya hoja yako......lakini tukija kwenye muktadha wa uharamu wa kughushi nyaraka ili ujipatie kitu.....inatoa uharamu wa malipo yote kwa ujumla......
Ni kweli kabisa mkuu, hela na mali yote ambayo imepatikana chini ya mwevuli wa kugushi cheti ni hela haramu kwa mhusika na ni mali ya serikali!
 
Mkuu inaelekea hata huijui maana ya haki.Haki ni "kile mtu anachostahili kuwa nacho au kile anachoruhusiwa kufanya, au kile anachostahili kupokea kutoka kwa wengine kwa mujibu wa sheria."

Naomba u-note maneno "kile mtu anachoruhusiwa kufanya" na "anachoruhusiwa kupokea kutoka kwa watu wengine kufuatana na sheria!"

Mkuu kufuatana na sheria "huruhusiwi kugushi cheti" na pia "huruhusiwi kupokea hayo malipo," kwa hivyo siyo haki yako.
 
Cheti ndicho kinacho prove kwamba mtu huyo ana-uwezo mkubwa mkuu,huo ndio mfumo tuliojiwekea kwa sasa,na sheria zetu zinatambua hivyo,so it must be respected.Kinyume chake ni kufanya kosa na sheria lazima ichukue mkondo wake.
 
Cheti haki-prove uwezo, kinaprove kwamba alisoma! Uwezo ni kitu kingine kabisa, Unaweza kuwa na cheti na usiwe na uwezo, pia kuna watu wana uwezo mkubwa sana lakini hawana vyeti!
 
Wametafuna michango ya wafanyakazi kwenye mifumo ya Jamii means ni hela za wanachama haikutakiwa kuguswa kabisa ni pesa za watu.Baada ya kuifilisi mifuko hii ndo wakaja na mpango wa kuiunganisha Ili hela zionekane nyingi na kuwafukuza watu Kazi Ili kuwazulumu michango yao.Hata kama waliwafukuza but ni sahihi walipwe michango yao si walishachanga.
 
Cheti ndicho kinacho prove kwamba mtu huyo ana-uwezo mkubwa mkuu,huo ndio mfumo tuliojiwekea kwa sasa,na sheria zetu zinatambua hivyo,so it must be respected.Kinyume chake ni kufanya kosa na sheria lazima ichukue mkondo wake.
Cheti sio tatizo.tatizo je alikisomea.Huwezi ukafoji professional
 
Cheti haki-prove uwezo, kinaprove kwamba alisoma! Uwezo ni kitu kingine kabisa, Unaweza kuwa na cheti na usiwe na uwezo, pia kuna watu wana uwezo mkubwa sana lakini hawana vyeti!
Mfano wachina awaamini kabisa katika vyeti, vyeti ni kama ID tu wao uamini katika weledi.Wanaamini kwamba mtu yeyeto mwenye akili timamu anaweza akafundwa taaluma au chochote na akamudu.
 
Mfano wachina awaamini kabisa katika vyeti, vyeti ni kama ID tu wao uamini katika weledi.Wanaamini kwamba mtu yeyeto mwenye akili timamu anaweza akafundwa taaluma au chochote na akamudu.
uongo kwa hiyo kule mtu yeyote aweza kuwa daktari wa operation au rubani bila cheti? vyuo vikuu wanafundisha wasio na vyeti?
 
Huyu lazima atakuwa mhanga wa vyeti feki....yaani

Sijaelewa mantiki ya hoja yako......lakini tukija kwenye muktadha wa uharamu wa kughushi nyaraka ili ujipatie kitu.....inatoa uharamu wa malipo yote kwa ujumla......
Kuna hukumu ya mahakama au tunatumia hisia za mhutu yule kuwa uamuzi wa haki?
 
uongo kwa hiyo kule mtu yeyote aweza kuwa daktari wa operation au rubani bila cheti? vyuo vikuu wanafundisha wasio na vyeti?
Tatizo lenu wazalendo wengi, hamna uelewa wa kimataifa! Vyeti ni vikaratasi tu, Unaweza kuwa nacho bado ukawa huna akili wala ujuzi unao takiwa! Wengi hapa kwetu wana vyeti kwa rushwa na rushwa ya ngono! Cheti kina heshima, kama mwenye nacho amepata ujuzi kwa alicho somea!
 
Mimi ninaowajua tu wako watatu, wana vyeti siyo vyao.

Wengine nimesoma nao secondary. Hata sasa kazini wanatambulika kwa majina yao ya kwenye vyeti.
 
Mimi sijazuia watu wasilipwe bali nimetoa tu maoni yangu kama wachangiaji wengine.....je ni dhambi kufanya hivyo.....?
Walipwe haki zao. Sisi tulipata huduma yao tena vizuri kabisa, hatujui hayo ya vyeti feki maana vyeti havikutuhudumia bali watu walituhudumia. Halafu nimegundua kuwa kumbe vyeti siyo kitu sana bali huduma ya mtu. Hawa bila ya hivyo vyeti walituhudumia vizuri kabisa!
 
Ni kweli kabisa mkuu, hela na mali yote ambayo imepatikana chini ya mwevuli wa kugushi cheti ni hela haramu kwa mhusika na ni mali ya serikali!
Vipi PhD feki iliyompatia mtu urais ? Vipi kura feki uchaguzi mkuu uliowapatia watu madaraka , kwahiyo urais uliopatikana kwa kudanganya elimu PhD na kuiba kura wenyewe sio haramu ? Mambo hayo sio mepesi Kama unavyofikiri .
 
Wewe muogope Mungu wako mbona Kuna mtu kughushi PhD na kaghushi matokeo ya uchaguzi wa rais , wabunge , madiwani , wenyeviti wa mitaa , vipi wenyewe wanastahili ? Wenyewe ndio wana haki sio ?
 
Huyu lazima atakuwa mhanga wa vyeti feki....yaani

Sijaelewa mantiki ya hoja yako......lakini tukija kwenye muktadha wa uharamu wa kughushi nyaraka ili ujipatie kitu.....inatoa uharamu wa malipo yote kwa ujumla......
Angalia michango yangu humu JF utajua mimi ni mtu wa namna gani ? Mimi kazi ni kupinga dhuluma na kutetea haki za watu wote , michango yangu mingi nimelaani Sana Utawala wa Jiwe kwa kukandamiza demokrasia , ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu , utawala bora, uhuru wa vyombo vya habari , utekaji , uuaji ufungaji wa watu kwenye viroba , mauaji ya watu uchaguzi wa serikali za mitaa , uchaguzi mkuu , mauaji ya uchaguzi mkuu wa Zanzibar , ubambikiaji wa kesi za uonezi za uhujumu uchumi , utakatishaji fedha , uporaji fedha kwenye bureau de change , akaunti za matajiri , kwahiyo haya yote nikiyoyapigania hapa juu mimi ni mhanga eti we tabulalasa ?
 
Ni kweli kabisa mkuu, hela na mali yote ambayo imepatikana chini ya mwevuli wa kugushi cheti ni hela haramu kwa mhusika na ni mali ya serikali!
Nyinyi hebu acheni propaganda , watumishi wote wale waliofukuzwa serikali haina sababu zozote zile za kutowalipa haki zao na stahiki zao , Kama walifoji kwanini Jiwe hakuwapeleka mahakamani ? Alijua na aliambiwa mengi kuliko mnayoyajua , ila kwa kuwa alikuwa anatafuta hela kununulia ndege akawafukuza ili achukue mishahara yao , mbona aliyewafukuza kafa kawaacha ?
 
uongo kwa hiyo kule mtu yeyote aweza kuwa daktari wa operation au rubani bila cheti? vyuo vikuu wanafundisha wasio na vyeti?
Hivi wewe huwa unaakili za namna gani wakunga waliokuwepo kwenye hospital za serikali wote walikuwa na uwezo kuliko manesi na madaktari , kabla daktari hajamzalieha lazima awaulize afanye nini pamoja na degree yake hasa madaktari fresh kidogo labda wakongwe uliza uambiwe experience worth much than certificate .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…