Rais Samia aagiza Mashirika ya Umma kuajiri Watumishi moja kwa moja

Rais Samia aagiza Mashirika ya Umma kuajiri Watumishi moja kwa moja

Rais kashauriwa vibaya sana kufanya uamuzi huo

ajira zikirudishwa kwmy Mamlaka za Mashirika maana yake tunarudisha Ajira za Mtoto wa Mjomba na shangazi
Hajasema mashirika yaajiri yenyewe, amesema ikitokea taasisi kama hizo zimeomba kibali basi PSRS wafanya haraka na sio kuwaachia mashirika yaajiri wenyewe.
Habari kama hii ni upotoshaji mkubwa.
 
Sekretarieti ya ajira (PSRS) wanacheleweshaga ajira bila sababu za msingi ilimradi tuu vikao vikao na posho za perdiem ziwe nyingi kwenye mchakato. Mfano kuna taasisi zinahitaji nguvu kazi na ziliomba watu tokea January 2022 lakini hadi leo psrs hawajawapelekea watu. Kazi zimetangazwa July 2022 usahili ukafanyika December na mpaka leo bado hawajachukua waliofaulu ili wapewe barua kwenda kwenye hizo taasisi. Taasisi zinaelemewa na majukumu na mwishowe zinaonekana hazina ufanisi na kazi hazikamiliki mwaka mzima kutokana na uhaba wa watumishi. Bora taasisi ziajiri zenyewe moja kwa moja hata kama kutakua na urasimu lakini watakaopata wataongeza mzunguko wa pesa mtaani kuliko hivi sasa
 
Ndio pale utumishi walikuwa hovyo sana wanajizungusha huku hayo mashirika yanalipa mishahara yenyewe .

Hapa TRA ,TANESCO na n.k wanakwenda kuajiri kwa speend tutegemee ajira za kutosha mitaani

USSR
View attachment 2517585
Mashirika yamekuwa yakiajiri siku zote sio jambo jipya mpaka mshangilie Ajira zitafanyika Shirika likuwa vizuri kiuchumi RAIS anatafuta KURA
 
Hii kitu ni hatari kupita maelezo.
Huko kwenye mashirika kumejaa upendeleo wa kiwango cha SGR, wakubwa wa hayo mashirika wataajiri wakwe, vimada, vijukuu, marafiki zao tupu.

Subiri uone kimbembe chake.
Hatari kweli kweli...
 
Amesemaje?

USSR
Amesema PSRS waharakishe mchakato wa upatikanaji wa waajiriwa wapya. Sio kibali kimetoka wao wanakaa muda mrefu wakati kibali kilichatolewa, acha kukurupuka.
 
Watoto wa walalahoi ndio msahau kupata kazi katika hizo taasisi. Utumishi sifahamu makando kando yao mengine ila kwenye suala la ajira wako fair sana. Ni kupitia mfumo wao wa ajira nimeona vijana waliotokea familia za kawaida (akina sie watoto wa mama ntilie) wakipata kazi mashirika/vitengo nyeti Serikalini. Rais Mama Samia Usijaribu kuua mende kwa nyundo, fikiria tena kuhusu kauli/maamuzi yako, elewa tatizo lilipo kisha tatua ila sio kwa kuondoa mfumo rasmi uliopo. Kati ya Mashirika yaliyoongoza kwa vi Memo kabla ya mfumo wa ajira kuwepo ilikua ni TTCL na hapo TRA, ofisi nzima ilikua inaongozwa na familia.
Huyu mama amekama serikalin lakini hajui lolote badala ya kujenga anaboma walioweka huo mfumo wa centralized sio wajinga walikaa wakaona mbali
 
Hajasema mashirika yaajiri yenyewe, amesema ikitokea taasisi kama hizo zimeomba kibali basi PSRS wafanya haraka na sio kuwaachia mashirika yaajiri wenyewe.
Habari kama hii ni upotoshaji mkubwa.
Chawa kama chawa .wew ndo unajua sana kwani mama ameongea kingereza
 
kuna Nyakati pale National Insurance Corporation ilikuwa kama Tukuyu hadi watu wakawa wanaongea kinyakyusa

Taasisi ya Elimu kuna wakati ilikuwa kama kitongoji cha Rombo
Ama TRA kulikuwa Moshi js imagine

Tume ile ya ajira kama ilikwamua hivi
Sasahivi hamna dominance ya watu flani sehemu flani
Ni cha wote na ni nzuri sana kwa upande wa kifursa kwa Watanzania wote
 
Huyu maza sijui kama anaelewa ANACHOFANYA. Nafuu ilipokuwa centralised na interviews walau watu walipatikana wazuri. Sasa hivi vyeti feki na undugunaization unarudi
Kujuana kulipotea
Yani kila mtu alipoteana
Hata utendaji ulikuwa mzuri sana
 
kuna Nyakati pale National Insurance Corporation ilikuwa kama Tukuyu hadi watu wakawa wanaongea kinyakyusa

Taasisi ya Elimu kuna wakati ilikuwa kama kitongoji cha Rombo
Hata ingekuwa mimi siwezi kuona wa'kwetu anahustle na vyeti anavyo
PSRS ilipunguza hata kulaumiana
Anyways kaona mbali labda
 
kuna Nyakati pale National Insurance Corporation ilikuwa kama Tukuyu hadi watu wakawa wanaongea kinyakyusa

Taasisi ya Elimu kuna wakati ilikuwa kama kitongoji cha Rombo
😂😂😂
 
Katika hili nampongeza sana Rais Samia kwa uwezo na ubunifu wake wa kutatua matatizo. Utumishi inakera lakini ni muhimu kuendelea kutumika kwenye ajira.

Mamlaka na taasisi zisipewe mamlaka ya kujiajiri bila mchakato wa ndani kuratibiwa na kusimamiwa na utumishi. Taasisi zipewe jukumu la kutangaza ajira na tarehe za usaili lakini jukumu la kusimamia mchakato mzima wa ajira wasipewe wao.
Hata wasipo pewa wao ila upigaji bado hupo
 
Kuna watu wengi humu ufahamu ni chini ya 30%.
Hata waliposimamia sekretarieti ya ajira bado hatua mucho ya usaili ma hr wa taasisi husika waliokuwa na mwanya wa kupenyeza ndugu zao kama wangekidhi sifa.
Mambo mengine ya kipumbavu, taasisi inaomba kibali kinapatikana miezi 4 mbele then mchakato wanatupiwa sekretarieti ya ajira . Nao mchakato unachukua miezi 4 tena
 
Acha zirudi kwa muda. Haiwezekan mtu anamaliza chuo anakaa miaka 10 hajaajiriwa. Nchi ya kuzimu au wapi??
 
Back
Top Bottom