The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 2,186
- 4,940
Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan, ameahidi kuwa endapo ataendelea kupewa ridhaa ya kuongoza katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, Serikali yake itatoa ajira mpya 12,000 katika sekta za afya na elimu.
Akihutubia maelfu ya wananchi leo Alhamisi, Septemba 11, 2025, katika mkutano wa kampeni wilayani Uyui mkoani Tabora, Samia amesema ndani ya siku 100 baada ya uchaguzi, Serikali itaajiri watumishi 5,000 wa afya na walimu 7,000.
Amewapongeza wananchi wa Uyui kwa ushirikiano katika miradi ya kijamii, akibainisha kuwa zaidi ya Sh8.2 bilioni zimetumika kujenga vituo vipya vya afya vitano, kuongeza zahanati kufikia 57 na kukabidhi magari matatu ya wagonjwa.
Katika elimu, amesema shule za sekondari zimeongezeka kutoka 27 hadi 34 na shule za msingi kutoka 154 hadi 182, huku idadi ya wanafunzi ikiongezeka kutoka 12,000 hadi 17,500 kutokana na sera ya elimu bila malipo.