Aramun
JF-Expert Member
- Nov 8, 2023
- 461
- 2,213
Kumekuchaje wanajamvi?
Wakati tukisubiria hukumu ya akina Nyundo Mjeda na wenzake dhidi ya Binti wa Yombo, hebu tumkumbushe mama kitu kimoja cha msingi maana huenda hajui.
Kwenye uongozi kuna mambo 2 ya msingi ambayo kwa kiongozi yeyote yule hata mjumbe wa nyumba 10 huwa hayakwepeki.
Mambo hayo mawili ni "Responsibility & Accountability" au kwa Kiswahili "Wajibu & Uwajibikaji".
Wajibu: Kama kiongozi, una jukumu la kuwa na mamlaka au udhibiti juu ya kitu au mtu fulani. Kama kiongozi una wajibu wa kufanya kazi fulani ili kufikia matokeo fulani.
Uwajibikaji: Ikiwa unawajibika kwa jambo fulani, utawajibishwa kwa matokeo ya kile kinachotoka humo, kwani huu ulikuwa ni wajibu wako. Kwa mifumo ya usimamizi wa ubora ni muhimu kwamba uwajibike kwa matendo yako.
Baada ya kuangalia hotuba yake ya juzi, nimesikitika sana kuona mama kama kiongozi namba 1 nchini "Kujitoa" kwamba hahusiki na mauaji yanayoendelea nchini.
Lakini akumbuke kwamba hakuna aliyemtupia lawama kwamba yeye ndiyo anaua. Ila yeye kama kiongozi alipaswa awe na majibu yanayoridhisha kwamba haya mauaji yanayoendelea ni kipi hasa kiini chake?
Suspects wakubwa wanaohusishwa na haya mauaji ni Jeshi la Polisi. Hiyo ni kutokana na "Scenes" za matukio zilivyo, pamoja na majibu na muitikio wa Jeshi la Polisi kwenye kufanya uchunguzi wa haya matukio. Yani raia waki-toss the coin, all odds zinawaangukia Jeshi la Polisi kuhusika kwa namna moja au ngingine!
Mama kama Amiri Jeshi Mkuu, Majeshi yote yako chini yake including Jeshi la Polisi! Kwenye kilele cha maadhimisho ya miaka 60 ya Jeshi la Polisi, hotuba ya mama ilionesha wazi kiwakingia kifua Polisi. Mama ali-side na wanaohisiwa kwamba wanahusika kwa namna moja ama nyingine na haya matukio ya mauaji!
Mama akumbuke baada ya kuuawa kwa Mzee Kibao, kilio cha wananchi ilikuwa iundwe tume huru kuchunguza haya mauaji. Jeshi la Polisi haliwezi kujichunguza kwani wananchi hawana imani nalo tena kwenye haya matukio ya namna hii. Ila mama siku hiyo hakutoa majibu ya kueleweka juu ya haya matukio!
Katika mazingira kama haya, mama kama namba moja anajitoaje?
Mama wajibu wake ni kuwawajibisha wale waliohusika na matendo haya ya mauaji. Huo ndiyo wajibu wake. Kinyume na hapo, akishindwa kuwawajibisha basi hili zigo la lawama lazima limuangikie yeye, yeye ndiyo inabidi abebe uwajibikaji kama kiongozi.
Walio karibu mkumbusheni mama yeye kama kiongozi ana Wajibu kwenye kila jambo linalowahusu wananchi wake, hiyo ni automatic, apende asipende.
Akishindwa kufanya Wajibu wake, kamwe pia hawezi kukimbia Uwajibikaji endapo mambo yataenda mrama kwenye jambo lolote lile linalowahusu wananchi.