Na mimi nakwambia hivi, masuala ya kimataifa ni masuala ya serikali ya muungano, si masuala ya serikali ya mapinduzi ya Zanzibar.
Ndiyo maana Salmin Amour alivyotaka kuiingiza Zanzibar kuwa mwanachama wa OIC kinyemela kukazuka mgogoro wa kikatiba mpaka akachomoa.
Unakumbuka?
Ulikuwa umezaliwa?
Sasa, kumpeleka rais wa Zanzibar katika mkutano wa kimataifa wakati kuna Rais wa Tanzania, kuna Makamu wa Rais wa Tanzania, kuna Waziri Mkuu wa Tanzania, kuna Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania, ni kuchanganya kazi.
Katika katiba kuna mambo yametajwa kuwa haya ni mambo ya muungano, yanatakiwa kufanywa na serikali ya muungano. Mahusiano ya kimataifa ni moja ya hayo.
Kumpa mtu anayeongoza serikali ya mapinduzi ya Zanzibar kazi za serikali ya muungano za kimataifa ni kuchanganya mambo.
Huyo Rais Samia kuna mambo anafanya anayajua mwenyewe, na yanaweza kuwa na matokeo mabaya sana.