Rais Samia aanza kutoa Fedha bilioni 75.98 kwa Vijana na Wanawake kupitia Halmashauri za Wilaya. Hii ni Fursa, tuchangamkie

Jibu swali acha porojo Samia ametoa wapi pesa?
Samia Suluhu Hassan ndiye Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ndiye anayetuvusha kwenda kwenye nchi ya Ahadi, badala ya kuuliza maswali unayojua majibu yake, Wahamasishe vijana wakachukue mikopo hii isiyo na riba ili tujenge uchumi wetu
 
Wewe umechukua huo mkopo? Ungekuwa umechukua ungekuwa busy na wala usingekuwa unashinda humu kusifu na kuabudu as if utafanya kazi hii ya kusifu na kuabudu miaka yako yote. Serikali zinabadilika, walikuwepo wenzio kina Musiba, sasa yuko wapi?
Punguza Jaziba MKANDAHARI, mimi sina sifa ya kuchukua kwa sababu ya umri, ndio maana nakushauri wewe kijana, tengeneza kikundi na Vijana wenzako mwende mkapewe Elimu juu ya mikopo ya uwezeshaji kiuchumi
 
Ivi ningependa niulize mfano mmepewa mkataba wa miaka miwili na muda umepita na deni halijaisha je hatua zipi zinafuata?
@ngakotecture hii ni mikopo ya Vikundi, ni mikopo rafiki na isiyo na riba, unapewa grace period, lakini yote kwa yote kuna Wataalam katika Halmashauri watakao kukusaidia kukupa ushauri
 
Halmashauri hizi hizi ambazo pesa ya mfuko wa jimbo inaingia lakini wanufaika ni wao wenyewe

Huku Kibaha Pangani barabara ya Halimashauri imejengwa chini ya kiwango . Hakuna wa kukagua ...

Huku Halimashauri ya mji wa Kibaha Mtakuja barabara iendayo machinjioni ni kichaka miaka 2 imepita haijasafishwa hata halafu unatuambia nini
 
Samia huyu maskini wa Zanzibar apate wapi hela zote hizo?
Vichwa vya ccm sijawahi kuvielewa. Pesa ni yetu wananchi. Pesa inapotoka si kushangilia kama watu hawajielewi, tushangilie only pale serikali inapoweza kuzisimamia maana huko kuna mchwa hatari
 
Hizo fedha zinatolewa kwa UVCCM na siyo vijana wote nchi hii.
Nilishashuhudia wana-CCM wakiitana serikali ya mtaa Salasala,Dar es salaam wakimwita jamaa yangu akachukue pesa japo hana Biashara yoyote.
@butron Huu uongo hausaidii kitu, badala ya kueneza chuki na uongo usio na maana, tengeneza kikundi mwende Halmashauri mtapewa Elimu ya ujasiliamali na kisha mtanufaika na mikopo hii isiyo na riba, mikopo hii ni kwa Vijana, Wanawake na Watu wenye ulemavu bila kujali itikadi ya mtu
 
Vyura99tu Ujumbe umeupata na itapendeza kama utakusanya vijana na kuwapa elimu juu ya mikopo hii ili waweze nufaika na hatimaye kuchangia kwenye ujenzi wa Taifa hili.
Unasema kuwakusanya!! Hivi wamekuwa mawe!! Kwa hivyo unawakusanya vikundi sijui? Je unawapa pesa wafanye Nini au ndio hao mnawaona wakiuza huko barabarani wakati Nyumbani ameamka hajanywa chai na hajui jioni atakula Nini na atalala wapi! Hiyo pesa inarudishwaje?
Ndio maana wenye dhamana wanapeana kiasi kikubwa kuwawezeaha wenzawao na bado hazirejeshwi. !
Twanga maji!!!
 
ndo maana mkuu nimeuliza je ikiwa upo nje ya mkataba halmashauri wanachukua hatua gani kwa wana kikundi?
Ndio maana nasisitiza bora mchaguane watu ambao mnajuana na mnajishughulisha kwa sababu mtu mmoja akiwa na mwenendo mbaya, presha mnapata wote.
 
Kwanini unaniita muongo ilihali aliyepewa mkopo ni jamaa yangu.Acheni kutetea ujinga, upuuzi wa huu mfuko inajulikana,ata DC wa Temeke alishafanya uchunguzi na kuibua madudu ya hizi pesa.
 
Kwanini unaniita muongo ilihali aliyepewa mkopo ni jamaa yangu.Acheni kutetea ujinga, upuuzi wa huu mfuko inajulikana,ata DC wa Temeke alishafanya uchunguzi na kuibua madudu ya hizi pesa.
butron ni kweli anaweza kuwa aliyepewa mkopo ni jamaa yako au ndugu kabisa, lakini hakupewa kwa sababu yeye ana kadi ya ACT au CHADEMA au CCM, kapewa kwa sababu moja ni Kijana wa Kitanzania, amejiunga na kikundi na anaenda kutumia mkopo kwaajili ya ujasiliamali,
Kwa sasa mikopo hii inatolewa kwa njia ya mfumo, kwahiyo hakuna udanganyifu unaoweza kufanyika
 
Issue ni kupata sisi wa chini yaani hio wanaipiga kwa connection, mkienda vijana ambao hamna connection hampati hata senti
antanarivo ya kale yashapita, jikusanyeni vijana azisheni biashara mkasajiliwe, muoneni Afisa Maendeleo wa eneo mlilopo awape elimu zaidi juu ya uwezeshwaji Wananchi kiuchumi, mikopo hii inaombwa kwenye mfumo hakuna ujanja ujanja wa zamani.
 
Ndio maana nasisitiza bora mchaguane watu ambao mnajuana na mnajishughulisha kwa sababu mtu mmoja akiwa na mwenendo mbaya, presha mnapata wote.
Uko sahihi kabisa Turudi pale Rau Madukani ni muhimu saana kwanza wote muwe mnabiashara au hata kama ndio mnaanza basi muwe mnajuana vizuri, mtu asije chukua then asitumie kwenye biashara, wakati wa kulipa mmoja akisumbua basi Wanakikundi wote mtalazimika kubeba jukumu la kuhakikisha mkopo unalipwa
 
Vyura99tu umepewa kichwa kikusaidie kufikiri na si vinginevyo.
 
Vichwa vya ccm sijawahi kuvielewa. Pesa ni yetu wananchi. Pesa inapotoka si kushangilia kama watu hawajielewi, tushangilie only pale serikali inapoweza kuzisimamia maana huko kuna mchwa hatari
Escrowseal1 Kwa sasa Serikali imeweza kusimamia kwa asilimia 100, mikopo hii inatolewa kupitiaa mifumo.
 
Asante,
 
Nina shida na huu mtazamo wa RAIS ATOA FEDHA.

Naomba kufahamu ukwasi binafsi wa Rais hadi awe anatoa hela hizo nje ya mfuko wa umma..

Je hizo hela zinaatikanaje?

Nani anazipangia matumizi?

Nani anazifanyia ukaguzi?

Rais anapokiwa amezitoa, yeye anafaidikiaje at the end?

Nauliza maswali haya kwa sababu kila waziri na kiongozi mteuliwa akisimama huongelea kuhusu pesa anazotoa rais.

Kama sivyo, basi tusiendeleze dhambi ya kumgombanisha Rais na pesa za umma
 
Msanii Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ndiye Amiri Jeshi Mkuu, ndiye kiongozi mkuu wa Serikali,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…