Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Rais Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuapisha viongozi mbalimbali wakiwemo Wakuu wa Mikoa katika Ikulu ya Dar es Salaam, leo Agosti Mosi, 2022. Ratiba inatarajiwa kuanza saa 10:30 Jioni.
====
Aliyozungumza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa Majaliwa wakati wa uapisho.
Rais anawaamini kuwa hamtamuangusha. Imani ya Rais Juu yenu inatuunganisha sote, kwa hiyo tushirikiane kutelekeza ilani na maagizo ya Rais. Maelekezo mengi ya msingi mtapewa kesho, siku ambayo mtakaa na Rais. Jukumu letu ni kupokea maelekezo na kuyatekeleza. Na Jukumu la Msingi ni kuwatumikia wananchi wa Tanzania.
Aliyoyazungumza Rais Samia
Nawashukuru watu walioshika nafasi zenu kabla ya teuzi kwa utendaji wao. Watendaji hao waliondoka kwa sababu mbalimbali. Lakini pia niwapongeze mlioapa kwa imani mliyopata kutoka serikalini.
Rais Samia amwambia Chalamila ni Mtundu
Rais amesema anatumaini Alex Chalamila amekua ndio maana amemrudisha katika cheo cha ukuu wa mkoa. Amesema Chalamila ni mtendaji mzuri lakini ni mtundu mno.
Chalamila aliwahi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza ambaye alitenguliwa siku chache baada ya kuapa kwake. Ambaye kwa sasa ameteuliwa tena kama Mkuu wa Mkoa.
Kama teuzi ni nzuri au mbaya ni mimi wa kulaumiwa
Rais amesema uteuzi huwa unapitia hatua nyingi ikiwemo baadhi ya watu kukaa na majina hayo kisha huleta majina ayaangalie ambayo pia huwapa watu wengine wahakiki majina hayo. Baada ya hatua hizo hatua za mwisho huwa ni kupitisha majina hayo.
Amesema kama ikitokea uteuzi umekuwa ni mbovu wa kulaumiwa ni yeye na pia yakiwa mazuri yeye ndio wa kuambiwa kuhusu teuzi hizo.
KAZI IENDELEE KWA VIWANGO VYAKO.
Rais amewataka wateule wake kuwa wasijibu tu kazi iendelee bila kuwa na viwango vya kazi anazozitaka. Amesema hana mchezo na fedha za umma. Amekumbusha kuwa aliwahi kusema wakitaka kujua rangi zake wacheze na fedha za umma 'Kuna wanaume walijaribu kuzijua rangi zangu' amesema
Amesema kuna mivutano mikubwa kati ya wakurugenzi, wakuu wa wilaya, wabunge, madiwani. Amesema wakuu wa wilaya sio kazi yao kuangalia fedha iende wapi bali kukubaliana na uamuzi wa bunge dogo(Uamuzi wa madiwani). Amesema hata wakati mwingine madiwani pia hugawika.
Amesema fedha ya umma ni kwa ajili ya wananchi hivyo waache mivutano ili isiendelee kukaa kwenye akaunti na kuchelewesha miradi.
VIWANGO VYA MAPATO MLIVYO PANGA NI VIDOGO
Rais amewaambia wateule viwango wanavyojiwekea ni vidogo kutokana na viwango vya nyuma. Amesema kuna haja ya watu kuweka viwango sahihi kutokana na maeneo waliyopo.
RAIS HANA RAFIKI, NA WATEULE WAKE WASIWE NA MARAFIKI
Rais amewakemea wateule wake tabia ya kuunda kundi la marafiki hali inayodhoofisha kazi ya kuwatumikia wananchi. Amesema rais hana rafiki, na wateule wake hawana rafiki. Rafiki wa rais ni mtu anayetenda kazi kwa weledi na anayesimamia wananchi. Ikigundulika mtu ametengeneza kundi la marafiki atapaswa kupisha na kukaa pembeni.
RAIS AMSHUKIA CHALAMILA
Rais amemwambia RC Chalamila aende tena akawaambie wananchi 'Andikeni tu'. Kauli ambayo aliitoa akiwa mkuu wa mkoa wa Mwanza kabla ya kutenguliwa. Hata hivyo Rais amesema mabango ni sauti ya wananchi na malalamiko yao hivyo si vyema kuyazuia maana kuzuia mabango ni kuzuia sauti za wananchi.
Rais amewakemea wateule wa mashirika kusimamia mapato. Amesema kuna watu wengine walikuwa wanakopa hela ili kuonesha mashirika yamezalisha wakati kiuhalisia hakuna walichozalisha.
Amewataka wateule kufanya kazi kwa uzuri, kwa kuwa wakifanya kazi vibaya atawatengua muda wowote ameshauri wajitahidi kutimiza walau miezi sita.