RAIS Samia Suluhu Hassan amemwagiwa sifa na wananchi na viongozi mbalimbali ndani na nje ya nchi kwa kuchukua hatua za haraka na madhubuti kushughulikia uzembe na ubadhirifu wa pesa za umma uliobainishwa kwenye ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).
Rais Samia amemuagiza Katibu Mkuu Kiongozi kuwaelekeza Makatibu Wakuu wote wa wizara pamoja na Watendaji Wakuu wa taasisi za serikali kusoma ripoti zote za CAG za mwaka wa fedha 2021/22 zilizotolewa hadharani Aprili 6 mwaka huu, kujibu na kuzifanyia kazi hoja zote zilizoibuliwa.
Hatua hizo za Rais Samia zimeibua shangwe za wananchi nchini Tanzania na hata kuwagusa wananchi wa nchi za jirani za Kenya na Uganda ambao wametoa maoni yao kupitia mitandao ya kijamii.