Rais Samia afanikisha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam tawi la Kagera kuanza kujengwa RC Mwassa asisitiza uharaka

Rais Samia afanikisha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam tawi la Kagera kuanza kujengwa RC Mwassa asisitiza uharaka

BWANKU M BWANKU

JF-Expert Member
Joined
Jan 12, 2019
Posts
377
Reaction score
435
Na Bwanku M Bwanku

🔨Kukamilika mwaka mmoja na nusu ujao, kwenda kufuta adha ya Mkoa wa Kagera kutokuwa na Chuo Kikuu.

Wiki iliyopita ilikua ya furaha na ndelemo baada ya Mkoa wa Kagera kuanza rasmi ujenzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Tawi la Kagera na kufuta changamoto ya mkoa wa Kagera kutokuwa na Chuo Kikuu hali inayosababisha Vijana wengi wa mkoa kusafiri umbali mrefu kwenda kusoma maeneo mengine. Baada ya miaka mingi ya mkoa kutokuwa na Chuo Kikuu, sasa Serikali ya Rais Samia imeamua kufuta hili.

Sasa rasmi Jumatano tarehe 30, 2024 Uzinduzi wa ujenzi wa mradi mkubwa sana wa ujenzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Tawi la Kagera ulizinduliwa rasmi kwa Mkandarasi Kampuni ya Kichina kukabidhiwa eneo la ujenzi wa mradi huo lililopo Kata ya Karabagaine, Tarafa ya Kyamtwara wilaya ya Bukoba.

Ujenzi wa mradi huo wa Chuo Kikuu utachukua miezi 18 na utagharimu zaidi ya Bilioni 20.

Mkuu wa Mkoa huo wa Kagera Mhe. Hajat Fatma Mwassa aliyeongoza mkutano huo mkubwa uliofurika wananchi wa kumkabidhi Mkandarasi eneo la ujenzi, amewashukuru wananchi wa Kata ya Karabagaine kwa kutoka hekari 315 kwa ajili ya ujenzi wa Chuo hiko huku akimsisitiza Mkandarasi kuhakikisha ujenzi unakamilika ndani ya muda uliopangwa ili wananchi waanze kunufaika na mradi huo mkubwa sana.

Naye, Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Mhe. Erasto Sima ambako mradi unatekelezwa amemhakikishia Mkandarasi pamoja na Makamu Mkuu wa Chuo hicho cha UDSM ambaye alikuwepo kwenye mkutano huo kwamba wilaya itatoa ushirikiano wote wakati zoezi la ujenzi wa Chuo hicho ukiendelea.

Kwa Mujibu wa Naibu Makamu Mkuu wa Chuo cha Dar es Salaam Prof. Bonaventure Rutinwa amesema kwa kuanza baada ya kukamilika, Chuo hicho kitatoa Kozi za biashara, masomo ya fedha na Kituo cha ujasiliamali kwa watu wote.
 

Attachments

  • 20240605_070157.jpg
    20240605_070157.jpg
    457.9 KB · Views: 8
  • IMG-20240604-WA0123.jpg
    IMG-20240604-WA0123.jpg
    22.7 KB · Views: 8
  • IMG-20240604-WA0122.jpg
    IMG-20240604-WA0122.jpg
    21.1 KB · Views: 7
  • IMG-20240604-WA0125.jpg
    IMG-20240604-WA0125.jpg
    23.5 KB · Views: 7
  • IMG-20240604-WA0124.jpg
    IMG-20240604-WA0124.jpg
    33.8 KB · Views: 9
  • IMG-20240604-WA0121.jpg
    IMG-20240604-WA0121.jpg
    22.3 KB · Views: 8
So kina ryeyemamu na rutashobya tutakua hatuna haja ya kuja darisalama kusoma UDSM. Na sisi tutakua tuna UDSM yetu huku huku BK!
 
Back
Top Bottom