Rais Samia afanya mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri. Angellah Kairuki aenda TAMISEMI, Balozi Mulamula atemwa, Bashungwa ahamishwa

Atamrudisha jaffo kwa kuchelewa mno. Unajua Jaffo na JK walikuwa hawakai pamoja.

Ila mama hana namna, hakuna atakayeiweza tamisemi zaidi ya jaffo ambaye alijitahidi kui shepu angalau. Hapo mama ndio amejisafisha kwa oil chafu kumuweka kairuki.
 
Mpaka wafie madarakani kila siku ni hao hao tu ni kubadilishwa unapelekwa huku, hivi huwa hamuwezi kuteua watu wapya mbona hata ndani ya CCM kuna watu wengi wenye sifa.
Endeleeni kupeana fadhila huku wengi wakilia, wakikumbuka usemi wa mwenda zake mh JPM mtanikumbuka, hakika dhambi hulipwa kwa dhambi hizi zote zitalipwa.
 
Kwamba hakuona wa kumpa hiyo nafasi hadi atuongeze mzigo mwingine wa kulipa mshara mbunge mwingine 🤔🤔🤔🤔🤔
 

Wizara ya TAMISEMI inatakiwa iwe na Waziri mkali sana.

Kiufupi inatakiwa Waziri wa TAMISEMI awe na 'roho mbaya' sana na asiwe na huruma dhidi ya wizi au uzembe unaopelekea mali ya Umma kupotea.
Sina hakika kama aliyetoka na aliyeteuliwa wana sifa hizo.

Labda ndani ya CCM kuna uhaba wa watu wanaofaa kuwa Mawaziri ama tunateuana kwa kuangalia kama tunajuana.

 
Hapa tumebadili chapati leo tunakula tambi kila cku ngano inatosha! 🙂
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…