Rais Samia afanya mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri. Angellah Kairuki aenda TAMISEMI, Balozi Mulamula atemwa, Bashungwa ahamishwa

Rais Samia afanya mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri. Angellah Kairuki aenda TAMISEMI, Balozi Mulamula atemwa, Bashungwa ahamishwa

Hivi mbunge akiteuliwa si anatakiwa kula kwanza kiapo cha ubunge?

Halafu, hadi sasa idadi ya wabunge wa kuteuliwa imefikia ngapi? Ukijumlisha wale wa JPM + 19 (Halima mdee et al)

Je, Mulamula anaendelea kuwa mbunge na kupokea posho za ubunge au anarudi kwenye nafasi yake ya hapo awali kabla ya uteuzi?
Amenyangaywa ubunge atakuwa balozi England

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Halafu, hadi sasa idadi ya wabunge wa kuteuliwa imefikia ngapi?
Hebu tuwataje walioteuliwa na rais:-
Mbarawa
Chamriho
Polepole
Bashiru
Stergomena
Mulamula
Angela Kairuki
...
......
......
.....
.......
.ongezeeni na ninyi
 
Hivi yule mzee aliyekua katibu mkuu TAMISEMI enzi za JPM, nafikiri jina lake ni Joseph Nyamhanga, akasimamia miradi kibao ambayo ndiyo inayozinduliwa sasa, mbona kama wamempotezea,

Kweli tenda wema nenda zako
Katibu mkuu tamisemi kipind hicho

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 

Wizara ya TAMISEMI inatakiwa iwe na Waziri mkali sana.

Kiufupi inatakiwa Waziri wa TAMISEMI awe na 'roho mbaya' sana na asiwe na huruma dhidi ya wizi au uzembe unaopelekea mali ya Umma kupotea.
Sina hakika kama aliyetoka na aliyeteuliwa wana sifa hizo.

Labda ndani ya CCM kuna uhaba wa watu wanaofaa kuwa Mawaziri ama tunateuana kwa kuangalia kama tunajuana.

Ikiwezekana rais mwenyewe awe tamisemi tuone

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom