Rais Samia afanya mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri. Angellah Kairuki aenda TAMISEMI, Balozi Mulamula atemwa, Bashungwa ahamishwa

Rais Samia afanya mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri. Angellah Kairuki aenda TAMISEMI, Balozi Mulamula atemwa, Bashungwa ahamishwa

Ni sahihi kabisa. Lazima kwanza ale kiapo cha kuwa Mbunge.

Hilo litawezekana, atakula kiapo katika ofisi ndogo za Bunge Dar es Salaam kisha kuwahi katika uapisho wa kuwa Waziri.
Kiapo ni bungeni Dodoma tu na ni ndani ya bunge
 
Tulishasema hapa kuhusu Bushungwa kuwa TAMISEMI haiwezi na ninasema tena huko kwenye wizara ya ulinzi ndiyo hapawezi kabisaa.
 
Stergomena alikuwa anasifiwa sana imekuwaje? Mulamula sidhani kama siasa anaziweza ila kihoja ni Bashungwa kuwa waziri wa ulinzi.
Hkn wizara rahis Kama ulinzi. Kule hakuhitaj makelele kila Kitu kinafanywa na vyombo vya ulinzi, we kusimamia sera tu. Huko kampeleka mwanae Kula bata. Aache kukimbizana na wakuu wa idara Huku vs wakurugenz
 
Nawaza kwamba ni kweli Kairuki ataiweza wizara ya TAMISEMI??
Nchi hii naona inauhaba sana wa watu wanazunguka walewale wanatenguana na kuteuana tena walewale ni kazunguko tu
Ningekua samia huyo kairuki angebadilishana na jafo. Jafo anaimudu sana TAMISEMI sema ndo hivyo rais akiona unakua maarufu kumzidi lazima akutoe hapo
 
Kwa Mulamula nadhani alizidi kupoa sana na Siasa inataka mashamsham haswa ya awamu hizi tokea JPM.

Naona kama Mama Tax ulinzi palimfaa zaidi lakini Bashungwa atakuwa ana nyota kali sana au kapiga maji yale ya ziwa victoria sio kwa kuaminiwa huko.

Ila Tamisemi mi naona Kairuki japokuwa aliwahi kufanya kazi huko enzinza nyuma lakini viatu hamvimtoshi. Plae palimfaa sana mtu kama Jafo, Polepole.
Jafo angefaa tatizo rais akiona unamzidi umaarufu anakutoa fasta.
 
Jafo angefaa tatizo rais akiona unamzidi umaarufu anakutoa fasta.
Jafo 2015-2020 mbona alifeli pakubwa. Mi naona hiyo wizara irudishwe chini ya waziri mkuu. TAMISEMI chini ya Jafo ilionekana vile kwa sababu mjomba ndo alifanya kila kitu ( kama waziri mwenye dhamana) lakini chini ya mama mwenye kuhitaji ughatuzi wa madaraka hakuna atakaeiweza. Ko ikisharudi chini ya waziri mkuu ndo atawajibika sana kama alivyofanya mjomba.
 
Ina maana kilio Cha wananchi walio wengi kwamba amtimue Mwigulu pale fedha hajakisikia?
 
Jafo 2015-2020 mbona alifeli pakubwa. Mi naona hiyo wizara irudishwe chini ya waziri mkuu. TAMISEMI chini ya Jafo ilionekana vile kwa sababu mjomba ndo alifanya kila kitu ( kama waziri mwenye dhamana) lakini chini ya mama mwenye kuhitaji ughatuzi wa madaraka hakuna atakaeiweza. Ko ikisharudi chini ya waziri mkuu ndo atawajibika sana kama alivyofanya mjomba.
Kila mmoja ana mtizamo wake mi binafsi utendaji wa jafo niliukubali awe chini ya OWM au OR
 
Mama inabidi ateue wananchi kuwa wabunge ndio awape uwaziri. Walioko bungeni kina Tale tale, Kaka Sanga, Nani yule muimbaji, Gwajima, Mdee utawala uwaziri gani???
 
Kwa Bashungwa naamini uchawi upo, huyu ndio alikuwa wa kufurusha
 
Back
Top Bottom