Rais Samia afanya mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri. Angellah Kairuki aenda TAMISEMI, Balozi Mulamula atemwa, Bashungwa ahamishwa

Rais Samia afanya mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri. Angellah Kairuki aenda TAMISEMI, Balozi Mulamula atemwa, Bashungwa ahamishwa

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri Kama ifuatavyo:

Amemteua Mhe. Dkt. Stergomena Lawrence Tax kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Awali Mhe. Dkt.Tax alikuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa. Aidha, Mhe. Tax anachukua nafasi ya Mhe. Balozi Liberata Mulamula.

Amemteua Mhe. Innocent Lugha Bashungwa kuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa. Awali Mhe. Bashungwa alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).

Amemteua Angellah Jasmine Kairuki kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Pia amemteua kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).

Mawaziri wote hao walioteuliwa wataapishwa tarehe 03 Oktoba, 2022 saa 3:00 asubuhi Ikulu Jijini Dares Salaam.

View attachment 2375256
Rais wangu Samia anatakiwa afanye kweli. Baraza Lake kwa sehemu kubwa haliko sawa. Anatakiwa kulibadilisha lote na sio kufanya hizi minor reshuffles! Hazitamsaidia lolote

Kuna watu ni mawaziri na manaibu waziri kwenye wizard ambazo hawana uwezo nazo kabisa sijui nini kinamfanya Rais wangu achelewe kufanya maamuzi.
 
Rais wangu Samia anatakiwa afanye kweli. Balaza Lake kwa sehemu kubwa haliko sawa. Anatakiwa kulibadilisha lote na sio kufanya hizi minor reshuffles! Hazitamsaidia lolote

Kuna watu ni mawaziri na manaibu waziri kwenye wizard ambazo hawana uwezo nazo kabisa sijui nini kinamfanya Rais wangu achelewe kufanya maamuzi.
Sio balaza ni baraza wewe kilaza. Alafu unasema baraza halipo sawa wewe Kama nan?
 
.
Screenshot_2022-10-02-22-59-40-89_40deb401b9ffe8e1df2f1cc5ba480b12.jpg
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri Kama ifuatavyo:

Amemteua Mhe. Dkt. Stergomena Lawrence Tax kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Awali Mhe. Dkt.Tax alikuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa. Aidha, Mhe. Tax anachukua nafasi ya Mhe. Balozi Liberata Mulamula.

Amemteua Mhe. Innocent Lugha Bashungwa kuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa. Awali Mhe. Bashungwa alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).

Amemteua Angellah Jasmine Kairuki kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Pia amemteua kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).

Mawaziri wote hao walioteuliwa wataapishwa tarehe 03 Oktoba, 2022 saa 3:00 asubuhi Ikulu Jijini Dares Salaam.

View attachment 2375256
Akijaga huku dar ndio anapewa majina na wahuni awateuwe na awateme nani...uuwiii 2025 ifike mapema. 🏃🏼‍♂️🏃🏼‍♂️
 
Hii nchi ina uhaba sana wa man power na ndio sababu wawekezaji wabakuja na wafanta kazi wao kutoka huko kwao then tunaanza lia lia, nchi imejaa recycle yaani mtu anatenguliwa baadae anakuja kuteuliwa tena.
 
Hivi mbunge akiteuliwa si anatakiwa kula kwanza kiapo cha ubunge?

Halafu, hadi sasa idadi ya wabunge wa kuteuliwa imefikia ngapi? Ukijumlisha wale wa JPM + 19 (Halima mdee et al)

Je, Mulamula anaendelea kuwa mbunge na kupokea posho za ubunge au anarudi kwenye nafasi yake ya hapo awali kabla ya uteuzi?
Ni sahihi kabisa. Lazima kwanza ale kiapo cha kuwa Mbunge.

Hilo litawezekana, atakula kiapo katika ofisi ndogo za Bunge Dar es Salaam kisha kuwahi katika uapisho wa kuwa Waziri.
 
Nawaza kwamba ni kweli Kairuki ataiweza wizara ya TAMISEMI??
Nchi hii naona inauhaba sana wa watu wanazunguka walewale wanatenguana na kuteuana tena walewale ni kazunguko tu
Inamaana Wabunge wote ndani ya CCM hakuna mwenye Uwezo wa kushika Wizara mpaka Raisi kaamua kuongeza mtu kutoka nje.
 
Kwa Mulamula nadhani alizidi kupoa sana na Siasa inataka mashamsham haswa ya awamu hizi tokea JPM.

Naona kama Mama Tax ulinzi palimfaa zaidi lakini Bashungwa atakuwa ana nyota kali sana au kapiga maji yale ya ziwa victoria sio kwa kuaminiwa huko.

Ila Tamisemi mi naona Kairuki japokuwa aliwahi kufanya kazi huko enzinza nyuma lakini viatu hamvimtoshi. Plae palimfaa sana mtu kama Jafo, Polepole.
 
Rais Mhe. SAMIA SULUHU HASSAN amefanya mabadiliko madogo katika Baraza lake la Mawaziri ambapo aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Liberata Mulamula ameondolewa katika nafasi yake, huku Mawaziri wengine wakibadilishwa wizara.
20221002_225120.jpg
 
Rais wangu Samia anatakiwa afanye kweli. Baraza Lake kwa sehemu kubwa haliko sawa. Anatakiwa kulibadilisha lote na sio kufanya hizi minor reshuffles! Hazitamsaidia lolote

Kuna watu ni mawaziri na manaibu waziri kwenye wizard ambazo hawana uwezo nazo kabisa sijui nini kinamfanya Rais wangu achelewe kufanya maamuzi.
Kati ya Dkt Stergomena na Mula nani ni mpole?
 
Back
Top Bottom