Rais Samia afanya mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri. Angellah Kairuki aenda TAMISEMI, Balozi Mulamula atemwa, Bashungwa ahamishwa

Rais Samia afanya mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri. Angellah Kairuki aenda TAMISEMI, Balozi Mulamula atemwa, Bashungwa ahamishwa

Rais wangu Samia anatakiwa afanye kweli. Baraza Lake kwa sehemu kubwa haliko sawa. Anatakiwa kulibadilisha lote na sio kufanya hizi minor reshuffles! Hazitamsaidia lolote

Kuna watu ni mawaziri na manaibu waziri kwenye wizard ambazo hawana uwezo nazo kabisa sijui nini kinamfanya Rais wangu achelewe kufanya maamuzi.
Kwani anayekuwa Rais ndio anapata na uwezo mkubwa wa akili na hekima kuliko wengine?
 

Attachments

  • FC8A308C-B350-4201-A93E-842023B1B779.jpeg
    FC8A308C-B350-4201-A93E-842023B1B779.jpeg
    29.7 KB · Views: 3
Unategemea jipya gani?
Pongezi kwa wote walio endelea kubaki.

Jambo la msingi wafanye kazi kwa bidii na kwa maarifa.

Wasijisahau kuwa Mama hufoka kwa KALAMU.........

Chapeni kazi, tatueni kero za wananchi kwani utendaji kazi kwa nia ya dhati bila unafiki ndio utakao wabeba, unafiki na uzandiki hauwezi kuwasaidia.
 
Hivi nchi hii hakuna watu wazuri kiutendaji zaidi ya hao, huyo Kairuki ana nini cha ziada?
 
Tofautisha RAIS na URAIS....umenielewa hapo mkuu?
Hakuna kitu kama hicho Raisi akiamua anaweza kumtengea waziri yoyote muda wowote alijisikia bila kushauriana na mtu yoyote katiba imempa nguvu Raisi, ata leo anaweza kumteua Makonda kuwa mbunge na kumpa uwaziri au anaweza kunichagua mimi kuwa mkuu wa mkoa na hakuna atakaye hoji.
 
Upo sahihi mkuu. Yaani Jiwe alikuwa rafiki sana na Baba yake bashungwa. Hivyo baba yake alilipenyeza jina lake kwa jiwe enzi hizo yaani kiufupi ni connection kati ya Baba inno na jiwe ndio ilimbeba Na huyo inno akatoka usa, kisha akazugazuga hapo wizarani kuna kazi fulani alikuwa nayo hapo na kampuni fulani hivi , huku mke wake alikuwa maarufu kama Mama alaska, halafu kupitia connection ya baba yake jamaa akawa mbunge wa karagwe, kisha waziri. Ndio mpaka leo hii.






Achana na Connection. Ni kitu kingine kabisa [emoji23][emoji23][emoji23]
Hivi Alaska imepotelea wapi? Maana bidhaa zake hazionekani wakati huu

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri Kama ifuatavyo:

Amemteua Mhe. Dkt. Stergomena Lawrence Tax kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Awali Mhe. Dkt.Tax alikuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa. Aidha, Mhe. Tax anachukua nafasi ya Mhe. Balozi Liberata Mulamula.

Amemteua Mhe. Innocent Lugha Bashungwa kuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa. Awali Mhe. Bashungwa alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).

Amemteua Angellah Jasmine Kairuki kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Pia amemteua kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).

Mawaziri wote hao walioteuliwa wataapishwa tarehe 03 Oktoba, 2022 saa 3:00 asubuhi Ikulu Jijini Dares Salaam.

View attachment 2375256
Huyo x wa Mwendazake ataweza kweli huko Tamisemi?

Na mashaka kutolewa kwa Bashungwa ni kutokana na kuwatimua wabadhirifu huko Tamisemi ila anajua aliyewateua.
 
Back
Top Bottom