Rais Samia afanya mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri. Angellah Kairuki aenda TAMISEMI, Balozi Mulamula atemwa, Bashungwa ahamishwa

Rais Samia afanya mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri. Angellah Kairuki aenda TAMISEMI, Balozi Mulamula atemwa, Bashungwa ahamishwa

Huyo kairuki toka nazaliwa ni Waziri, tanganyika mnafeli wap kukosa mbadala huyo mama ana jipya gani kuisaidia nchi baada ya miaka yote hiyo kufeli?
 
Bado bashungwa hatoshi kwenye hiyo wizara, hiyo wizara Inahitaji mtu kazi ambaye yupo seriously bashungwa namuona laini laini sn
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri Kama ifuatavyo:

Amemteua Mhe. Dkt. Stergomena Lawrence Tax kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Awali Mhe. Dkt.Tax alikuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa. Aidha, Mhe. Tax anachukua nafasi ya Mhe. Balozi Liberata Mulamula.

Amemteua Mhe. Innocent Lugha Bashungwa kuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa. Awali Mhe. Bashungwa alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).

Amemteua Angellah Jasmine Kairuki kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Pia amemteua kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).

Mawaziri wote hao walioteuliwa wataapishwa tarehe 03 Oktoba, 2022 saa 3:00 asubuhi Ikulu Jijini Dares Salaam.

View attachment 2375256
nchi hii tabu tupu. Ukipoata nafasi IBA kwa kwenda mbele maana hujui kama kesho utakuwepo johnthebaptist
 
Bado bashungwa hatoshi kwenye hiyo wizara, hiyo wizara Inahitaji mtu kazi ambaye yupo seriously bashungwa namuona laini laini sn
Ina kitu gani cha zaidi? CDF ndiye anaamua kila kitu, Waziri ni ceremonial, I can say!
 
Hivi mbunge akiteuliwa si anatakiwa kula kwanza kiapo cha ubunge?

Halafu, hadi sasa idadi ya wabunge wa kuteuliwa imefikia ngapi? Ukijumlisha wale wa JPM + 19 (Halima mdee et al)

Je, Mulamula anaendelea kuwa mbunge na kupokea posho za ubunge au anarudi kwenye nafasi yake ya hapo awali kabla ya uteuzi?
Rais yuko juu ya katiba na sheria zake. Hivyo anaweza fanya loloteeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee
 
Rais wangu Samia anatakiwa afanye kweli. Baraza Lake kwa sehemu kubwa haliko sawa. Anatakiwa kulibadilisha lote na sio kufanya hizi minor reshuffles! Hazitamsaidia lolote

Kuna watu ni mawaziri na manaibu waziri kwenye wizard ambazo hawana uwezo nazo kabisa sijui nini kinamfanya Rais wangu achelewe kufanya maamuzi.
Kama akina nani?
 
Hivi yule mzee aliyekua katibu mkuu TAMISEMI enzi za JPM, nafikiri jina lake ni Joseph Nyamhanga, akasimamia miradi kibao ambayo ndiyo inayozinduliwa sasa, mbona kama wamempotezea,

Kweli tenda wema nenda zako
Kama miradi ipi hiyo?
 
Huyu mvaa tai ya bendera kamuachaje licha ya kelele za watozwa tozo? Basi sawa, acha Ile kauli ya Hichilema wa kule Zambia ijisimike vyema!
Kwamba kelele za Chadomo ndio base ya Rais kufanyia maamuzi? Acha uzwazwa..

Ni hivi Mwigulu toka enzi za JK huyo,Simbachawene,Jenista hao ni senior ministers hawatoki Leo wala kesho na Sasa Bashungwa anaingia kwenye hiyo Orodha.
 
Mganga wa Dk. Mwigulu Nchemba si wa mchezo mchezo kwani Kaupiga mwingi kwa Ndumba na Mama Kamsahau kabisa Kumtumbua.
Mama anamuamini Mwigulu hata tone ya anapomzungumzia au Mwigulu anapomzungumzia Rais unaweza Iona..

Kwa hiyo Chuki zenu haziwezi kuwasaidia kitu,hakuna cha mganga Wala nani..

Mwisho unapomshutumu mtu uje Kwa figures kuonyesha kwamba ameharibu Uchumi ila kama uchumi unakua na pesa za miradi zinapatikana,shutuma zenu zinasalia kuwa kelele za chuki binafsi na mtapuuzwa..

Kwa mara ya Kwanza Mwigulu amesimamia utekelezaji wa Bajeti Kwa zaidi ya 95%,haijawahi tokea.
 
Atamrudisha jaffo kwa kuchelewa mno. Unajua Jaffo na JK walikuwa hawakai pamoja.

Ila mama hana namna, hakuna atakayeiweza tamisemi zaidi ya jaffo ambaye alijitahidi kui shepu angalau. Hapo mama ndio amejisafisha kwa oil chafu kumuweka kairuki.
Jafo hawezi kurudi tena Tamisemi..Arudi ili hati chafu zirudi au? By the way Bashungwa amefanya Kazi nzuri Tamisemi kuanzia mapato kuongezeka hadi kutimua majizi.
 
Back
Top Bottom