Rais Samia Suluhu Hassan amewasili katika Viwanja vya Makazi ya Rais (Bogor Presidential Palace) Jijini Jakarta, Indonesia na kupokelewa na mwenyeji wake Rais Joko Widodo ikiwa ni sehemu ya ziara ya siku mbili nchini hapo.
Rais Joko Widodo ambaye alifanya ziara Nchini Tanzania, Agosti 2023 amempa mwaliko Rais Samia ikiwa ni mwendelezo wa ushirikiano wa Kidiplomasia baina ya Nchi hizo.
Your browser is not able to display this video.
Viongozi hao wawili wameshuhudia Mabadilishano ya Hati za Makubaliano (4) na Barua ya Kusudio (1) vikiwa zinagusa Sekta za Uchumi wa Buluu, Kilimo, Madini, Diplomasia na Uwekezaji.
HATI ZA MAKUBALIANO ZILIZOSAINIWA
- Rasimu ya Hati ya Makubaliano kuhusu Ushirikiano katika Nyanja ya Uchumi wa Buluu
- Hati ya Makubaliano kuhusu Ushirikiano katika Sekta ya Kilimo
- Hati ya makubaliano kati ya Serikali ya Tanzania na Serikali ya Indonesia kuhusu Ushirikiano katika Sekta ya Madini.
- Hati ya Makubaliano kati ya Wizara ya Mambo ya Nje Tanzania and Wizara ya Mambo ya Nje Indonesia kuhusu Ushirikiano wa Kujengeana Uwezo katika Masuala ya Kidiplomasia.
- Rasimu ya Barua ya Kusudio kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Jamhuri ya Indonesia kuhusu kukuza na kuwezesha Uwekezaji
- Hati ya Makubaliano kati ya Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTDADE) na PT Perusahaan Perdagangan Indonesia
- Hati ya Makubaliano kati ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Chuo cha Teknolojia cha Bangung
HATI ZA MAKUBALIANO ZA SEKTA BINAFSI (PRIVATE SECTOR MoU’s)
- Hati ya Makubaliano kati ya Chemba ya Biashara, Viwanda na Kilimo ya Tanzania, Chemba ya Taifa ya Biashara ya Zanzibar na Chemba ya Biashara na Viwanda ya Indonesia.
KUTOA NENO KWA WANAHABARI
Rais Samia akizungumza na Waandishi wa Habari amesema makubaliano hayo yataimarisha miaka 60 ya kidiplomasia na uchumi.
Miongoni mwa masuala waliojadili viongozi hao ni namna ya kuimarisha uhusiano wa kibiashara na uwekezaji ambapo Tanzania ipo tayari kuwa mwenyeji wa mkutano wa kwanza wa tume ya Makubaliano ya ushirikiano.
Pia kumekuwa na majadiliano ya namna ya kuendeleza ushirikiano katika uwekezaji kwenye sekta ya mafuta na gesi huku kampuni ya Indonesia ya Pertamina ikiongeza hisa Mnazi Bay, Mtwara.
Mbali na kujenga uwezo kwa wafanyakazi wa TPDC, pia Indonesia ina nia ya kampuni yake ya ESSA kuwekeza kwenye kilimo hususan mbolea na Medco Energi kwenye upande wa nishati.
Upande wa sekta ya dawa, kipaumbele hasa ni Indonesia kuiuzia Tanzania dawa ambapo kwa kuanzia zitakuwa za saratani.
Aidha, kutokana na viongozi hao kushiriki kupanda mti, Rais Samia amesema hiyo ni ishara ya kuonesha kujali na kulinda mazingira.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akisaini Kitabu cha wageni mashuhuri mara baada ya kuweka shada la maua kwenye mnara wa kumbukumbu ya Makaburi ya Mashujaa ya Kalibata wakati wa ziara yake ya Kitaifa Jakarta nchini Indonesia tarehe 25 Januari,2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akiwapungia mkono Waandishi wa Habari pamoja na Mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Indonesia, Joko Widodo mara baada ya kuwasili katika Ofisi za Rais huyo Bogor Presidential Palace nchini humo tarehe 25 Januari, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akiteta jambo na Mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Indonesia, Joko Widodo kabla ya kwenda kupanda mti wa kumbukumbu katika viwanja vya Makazi ya Rais huyo Bogor Presidential Palace tarehe 25 Januari, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akiwa na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Indonesia, Joko Widodo wakati akipanda mti wa kumbukumbu mara baada ya kupokewa Rasmi katika viwanja vya Makazi ya Rais huyo Bogor Presidential Palace tarehe 25 Januari, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Indonesia, Joko Widodo katika Ofisi za Rais huyo Bogor Presidential Palace tarehe 25 Januari, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akiongoza ujumbe wa Tanzania kwenye mazungumzo Rasmi na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Indonesia, Joko Widodo pamoja na ujumbe wake katika Ofisi za Rais huyo Bogor Presidential Palace tarehe 25 Januari, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Indonesia, Joko Widodo katika Ofisi za Rais huyo Bogor Presidential Palace tarehe 25 Januari, 2024.
Asante sana kwa taarifa hii, JF is doing a very good job!.
Hapa JF ni funga kazi!, hakuna loca mainstream TV yoyote ya Tanzania wala online TV yoyote ya Bongo ambayo inaitangaza live ziara hii ya Rais Samia nchini Indonesia, hii maana yake ni JF ni zaidi ya mainstream TV, ni zaidi ya Redio yoyote, gazeti lolote, na online media yoyote ya Tanzania!, Big Up sana JF for this!.

Mkuu ni kweli, nakumbuka those good old days, enzi zile, ningekuwepo, sasa mambo yamebadilika, sisi sasa tumepitwa na wakati kuna madogo wa new media, wako kwenye multimedia, na online, sisi tumekuwa zilipendwa!.
Asante sana kwa taarifa hii, JF is doing a very good job!.
Hapa JF ni funga kazi!, hakuna loca mainstream TV yoyote ya Tanzania wala online TV yoyote ya Bongo ambayo inaitangaza live ziara hii ya Rais Samia nchini Indonesia, hii maana yake ni JF ni zaidi ya mainstream TV, ni zaidi ya Redio yoyote, gazeti lolote, na online media yoyote ya Tanzania!, Big Up sana JF for this!.
FAIDA YA ZIARA YA RAIS SAMIA SULUHU HASASAN INCHINI INDONESIA
1. Kukamilisha mazungumzo ya kuongeza ushiriki wa uwekezaji wa TPDC kwenye kitalu cha gesi Mnazi Bay mkoani Mtwara, ili kuongeza hisa na umiliki zaidi wa TPDC kwenye kitalu hicho kutoka 20% za sasa hadi 40%.
2. Kufungua fursa kwa sekta binafsi kupitia Kongamano la Biashara na Uwekezaji kwa lengo la kuvutia uwekezaji wenye thamani ya Dola za Marekani Bilioni 1 katika kipindi cha miaka mitano ijayo. Indonesia ni moja kati ya nchi 20 zenye uchumi mkubwa duniani (G20).
3. Kuvutia uwekezaji wa kuongeza thamani ya mazao yanayolimwa nchini ikiwemo karafuu na michikichi.
4. Kuanzisha ushirikiano baina ya Tanzania na Indonesia kwenye sekta ya uchumi wa buluu.
5. Kuanzisha mashirikiano ya utalii utakaowezesha kubadilishana uzoefu na kuvutia uwekezaji kwenye miundombinu ya utalii.