Rais Samia afanya uteuzi. Katibu Mkuu Kiongozi ahamisha Vigogo 5 TANESCO

Rais Samia afanya uteuzi. Katibu Mkuu Kiongozi ahamisha Vigogo 5 TANESCO

Hivi punde

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2017
Posts
2,554
Reaction score
8,587
Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Maharage Chande kuwa Mkurugenzi Mkuu wa TANESCO, akichukua nafasi ya Dkt. Tito Mwinuka

Kabla ya uteuzi huo, Chande alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Multichoice Afrika Kanda ya Afrika Mashariki na Magharibi

Vilevile, Rais Samia amemteua Omari Issa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya TANESCO

====

Rais Samia amemteua Hassan Seif Said kuwa Mkurugenzi Mkuu Wakala wa Nishati Vijijini (REA). Kabla ya uteuzi, alikuwa Meneja wa Kanda Mwandamizi wa Kanda ya Mashariki TANESCO

Aidha, Michael Minja ameteuliwa kuwa Kamishna wa Petrol na Gesi, Wizara ya Nishati. Kabla ya kuteuliwa, Minja alikuwa Mkurugenzi Mkuu TIPPER

Vilevile, Rais amemteua Felschemi Mramba kuwa Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu

=====

Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Hussein Kattanga amewahamisha Watumishi Waandamizi watano kutoka TANESCO kwenda Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora ambapo watapangiwa majukumu mengine

Waliohamishwa ni Naibu Mkurugenzi Mtendaji Uwekezaji, Khalid James; Naibu Mkurugenzi Mtendaji Usambazaji na Masoko, Mhandisi Raymond Seya na Naibu Mkurugenzi Mtendaji Usafirishaji, Mhandisi Isaac Chanje

Wengine ni Nyelu Mwamaja (Mkuu wa Kitengo cha Ununuzi) na Amos Ndegi (Mwanasheria wa TANESCO)

20210925_173524.jpg

20210925_173520.jpg


Pia, soma: Rais Samia Suluhu Hassan afanya uteuzi wake wa kwanza Ikulu. Gerson Msigwa atolewa Ikulu, Dotto James ahamishwa. TPA, TCRA na TRA zapata wakuu wapya
 
Huu uteuzi kaufanya Bw. Jan, hapo SSH jina lake limetumika tu. Wengi hapo ni marafiki wa Jan na atakuwa kawapanga makusudi kwa kazi maalum kujipanga na mtanange 2025 (kukusanya pesa).

Tusubiri visa na vituko kwenye umeme hadi pesa ipatikane. Fisi kapewa bucha.
 
Inshallah Mungu yupo tuwape muda na hawa pia tuone utendaji kazi wao pole hongera Tito mwinuka ulifunikwa na Kale Man nenda kapumue
 
Back
Top Bottom