Acha kujilisha upuuzi
Mramba aliondolewa baada ya tanesco kuwasilisha pendekezo la ongezeko la tarrif la 8%,
Aliyekuwa waziri wa Nishati kipindi hiko Prof Muhongo alitengua mapendekezo hayo na January 2017 Mramba akaondolewa kisha Dr Mwinuka ndio akateuliwa
Sasa na huyó Dr Mwinuka alikuwa Msukuma!???
Unaposema Jpm aliwachukia wachaga, je hufahamu kuwa Prof Adolph Mkenda aliteuliwa na Jpm kuwa katibu mkuu viwanda na biashara,,,, Je huyu Mkenda sio kutoka Jamii ya mkoa wa Kilimanjaro
Na ingekuwa ana chuki hiyo, je idara nyeti kama ya Mkurugenzi Mkuu TISS angewekwa bw Msuya!???
Washauri ndugu na Jamii yako wawe waadilifu, wasiwe wezi wezi na watu wa 'kitu kidogo' ili wasije kukumbwa na mkono wa kiongozi mwenye kutaka waadilifu
Leo hii kiongozi wa Serikali akifanya maamuzi ya kuwaondoa ombaomba mjini, basi kama tutaangalia kwa muktadha wa kabila lipi litakaloathirika sana basi ni wagogo, na ndio wataanza kumchukia na kusema huyu kiongozi hatupendi sisi wagogo