Makanyaga
JF-Expert Member
- Sep 28, 2007
- 11,129
- 7,321
MJADALA ULIHUSU NINI VILE?š¤£
Hii inazima mjadala wa TRA na CBE
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
MJADALA ULIHUSU NINI VILE?š¤£
Hii inazima mjadala wa TRA na CBE
Yaliyojiri kwa ndevuMJADALA ULIHUSU NINI VILE?
Haya mambo Yana siasa ndani yake,NAFASI YA WHO NI NZURI SANA LAKINI SITATAMANI KABISA JANABI AONDOKE MUHIMBILI MUDA HUU
MPOKI ULISUBISYA ANAFAA SANA KUGOMBEA NAFASI HIYO.
TAFADHALI SANA JANABI ASIONDOKE MUHIMBILI WAKATI HUU
Kabla ya uteuzi huu, Jerry silaa alikuwa wizara ipi?
Yule anayejiita Dr Jafo ameelekea wapi!
Series yake ya uteuzi ikianza ni mpaka uchaguziMahangaiko matupu
Sinema zetu.....hakika ni za kwetuKama mchezo wa draft tuu
Mvuvi yule. Sema kwa ngazi ya uwaziri sidhani kama taaluma ni jambo la msingi.Abdalah Hamis Ulega amesomea nini??
Labda wameona kuna kitu anaweza offer.Kabudi tena? Bashungwa mambo ya ndani na palivyo pagumu sasa hivi ataweza kweli? Ngoja tuone
Aisee!Kumpiga chini Rais mtarajiwa wa Zanzibar sio kazi rahisi
Ameteuliwa katika kipindi kigumu sana, anyway sometimes luck is better than goodBashungwa anaenda kuchafuliwa Sasa na mbio zake za urais 2025 ndio Basi tena
Bashungwa anaenda kuchafuliwa Sasa na mbio zake za urais 2025 ndio Basi tena
Mteule, mwingine huyu hapa!Wakuu,
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi na mabadiliko ya Viongozi mbalimbali.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. Moses Kusiluka, uteuzi na mabadiliko ya viongozi hao ni kama ifuatavyo:-
(i) Mhe. Rais Dkt. Samia amehamisha majukumu ya sekta ya habari kutoka Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kwenda Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo ambapo Mhe. Prof. Palamagamba John Aidan Mwaluko Kabudi (Mb.) ameteuliwa kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo;
(ii) Mhe. Jerry William Silaa (Mb.) ameteuliwa kuwa Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari
(iii) Mhe. Dkt. Damas Daniel Ndumbaro (Mb.) ameteuliwa kuwa Waziri wa Katiba na Sheria
(iv) Mhe. Mhandisi Hamad Yusuf Masauni (Mb.) ameteuliwa kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira);
(v) Mhe. Dkt. Ashatu Kachwamba Kijaji (Mb.) ameteuliwa kuwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi;
(vi) Mhe. Abdallah Hamis Ulega (Mb.) ameteuliwa kuwa Waziri wa Ujenzi;
(vii) Mhe. Innocent Lugha Bashungwa (Mb.) ameteuliwa kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi;
(viii) Bw. Gerson Msigwa ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali;
(ix) Dkt. James Henry Kilabuko ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu)
(x) Dkt. Stephen Justice Nindi ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Kilimo anayeshughulikia masuala ya ushirika na umwagiliaji;
(xi) Dkt. Suleiman Hassan Serera amehamishwa kutoka Wizara ya Kilimo kwenda kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Viwanda na Biashara.Aidha, Balozi Dkt. John Stephen Simbachawene atapangiwa kituo cha kazi;
(xii) Prof Mohamed Yakub Janabi ameteuliwa kuwa Mshauri wa Rais Masuala ya Afya na Tiba. Aidha, pamoja na nafasi hiyo Prof. Janabi ataendelea kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili
(xiii) Bw. Anderson Gukwi Mutatembwa ameteuliwa kuwa Balozi na atapangiwa kituo cha kazi;(xiv) Bw. Mobhare Matinyi ameteuliwa kuwa Balozi na atapangiwa kituo cha kazi;
(xv) Kamishna wa Polisi Zanzibar CP. Hamad Khamis Hamad ameteuliwa kuwa Balozi na atapangiwa kituo cha kazi;
(xvi) Kamishna wa Polisi CP. Suzan Kaganda ameteuliwa kuwa Balozi na atapangiwa kituo cha kazi;
(xvii) Bw. Thobias Makoba aliyekuwa Msemaji Mkuu wa Serikali ameteuliwa kuwa Balozi na atapangiwa kituo cha kazi.
Uapisho wa Viongozi walioteuliwa utafanyika Ikulu Ndogo, Tunguu Zanzibar tarehe 10 Desemba, 2024 kuanzia saa 5.00 asubuhi.