Rais Samia afanya uteuzi: Masauni aondolewa Wizara ya Mambo ya ndani, Kabudi apelekwa Wizara ya Habari na Michezo, Janabi kuwa mshauri wa Rais

Rais Samia afanya uteuzi: Masauni aondolewa Wizara ya Mambo ya ndani, Kabudi apelekwa Wizara ya Habari na Michezo, Janabi kuwa mshauri wa Rais

NAFASI YA WHO NI NZURI SANA LAKINI SITATAMANI KABISA JANABI AONDOKE MUHIMBILI MUDA HUU

MPOKI ULISUBISYA ANAFAA SANA KUGOMBEA NAFASI HIYO.

TAFADHALI SANA JANABI ASIONDOKE MUHIMBILI WAKATI HUU
Haya mambo Yana siasa ndani yake,
Hivi kabla ya kifo Cha Ndungulile, ulikuwa unaojua ni family friend na Mzee Kikwete?

Kwamba Mzee Kikwete alifanya kazi na babaake Ndungulile Foreign Affairs,
 
Janabi aanze na bajeti ya chakula pale ikulu, pakti moja ya karanga wanakula watu wawili, na maji ya kuchemsha
 
Naona shemeji yetu anaendelea na tamisemi yake ili uchaguzi mkuu afanye yale aliofanya kwenye uchaguzi wa serekali za mitaa.
 
Bashungwa anaenda kuchafuliwa Sasa na mbio zake za urais 2025 ndio Basi tena
Licha ya ukweli kwamba hakuna mtu ataiweza wizara ya mambo ya ndani kama atakubaliana na vya kunyonga vya CCM, Bashungwa bado yupo mbali sana na Urais.
 
Wakuu,

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi na mabadiliko ya Viongozi mbalimbali.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. Moses Kusiluka, uteuzi na mabadiliko ya viongozi hao ni kama ifuatavyo:-

(i) Mhe. Rais Dkt. Samia amehamisha majukumu ya sekta ya habari kutoka Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kwenda Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo ambapo Mhe. Prof. Palamagamba John Aidan Mwaluko Kabudi (Mb.) ameteuliwa kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo;

(ii) Mhe. Jerry William Silaa (Mb.) ameteuliwa kuwa Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari

(iii) Mhe. Dkt. Damas Daniel Ndumbaro (Mb.) ameteuliwa kuwa Waziri wa Katiba na Sheria

(iv) Mhe. Mhandisi Hamad Yusuf Masauni (Mb.) ameteuliwa kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira);

(v) Mhe. Dkt. Ashatu Kachwamba Kijaji (Mb.) ameteuliwa kuwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi;

(vi) Mhe. Abdallah Hamis Ulega (Mb.) ameteuliwa kuwa Waziri wa Ujenzi;

(vii) Mhe. Innocent Lugha Bashungwa (Mb.) ameteuliwa kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi;

(viii) Bw. Gerson Msigwa ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali;

(ix) Dkt. James Henry Kilabuko ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu)

(x) Dkt. Stephen Justice Nindi ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Kilimo anayeshughulikia masuala ya ushirika na umwagiliaji;

(xi) Dkt. Suleiman Hassan Serera amehamishwa kutoka Wizara ya Kilimo kwenda kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Viwanda na Biashara.Aidha, Balozi Dkt. John Stephen Simbachawene atapangiwa kituo cha kazi;

(xii) Prof Mohamed Yakub Janabi ameteuliwa kuwa Mshauri wa Rais Masuala ya Afya na Tiba. Aidha, pamoja na nafasi hiyo Prof. Janabi ataendelea kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili

(xiii) Bw. Anderson Gukwi Mutatembwa ameteuliwa kuwa Balozi na atapangiwa kituo cha kazi;(xiv) Bw. Mobhare Matinyi ameteuliwa kuwa Balozi na atapangiwa kituo cha kazi;

(xv) Kamishna wa Polisi Zanzibar CP. Hamad Khamis Hamad ameteuliwa kuwa Balozi na atapangiwa kituo cha kazi;

(xvi) Kamishna wa Polisi CP. Suzan Kaganda ameteuliwa kuwa Balozi na atapangiwa kituo cha kazi;

(xvii) Bw. Thobias Makoba aliyekuwa Msemaji Mkuu wa Serikali ameteuliwa kuwa Balozi na atapangiwa kituo cha kazi.

Uapisho wa Viongozi walioteuliwa utafanyika Ikulu Ndogo, Tunguu Zanzibar tarehe 10 Desemba, 2024 kuanzia saa 5.00 asubuhi.


Mteule, mwingine huyu hapa!
Sijajua Huwa anashauriwa na nani!!
 

Attachments

  • IMG-20241208-WA0022.jpg
    IMG-20241208-WA0022.jpg
    109 KB · Views: 3
Back
Top Bottom