Rais Samia afanya uteuzi mpya wa Wakili Mkuu wa Serikali na Naibu wake, leo Oktoba 10, 2022

Rais Samia afanya uteuzi mpya wa Wakili Mkuu wa Serikali na Naibu wake, leo Oktoba 10, 2022

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa Wakili Mkuu wa Serikali na Naibu Wakili Mkuu wa Serikali kama ifuatavyo:
  • Amemteua Dkt. Boniphace Christopher Luhende kuwa Wakili Mkuu wa Serikali. Kabla ya uteuzi huu Dkt. Luhende alikuwa Naibu Wakili Mkuu wa Serikali. Dkt. Luhende anachukua nafasi ya Bwana Gabriel Paschal Malata ambaye aliteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu.​
  • Amemteua Bi. Sarah Duncan Mwaipopo kuwa Naibu Wakili Mkuu wa Serikali. Kabla ya uteuzi huu Bi. Mwaipopo alikuwa Wakili wa Serikali Mkuu katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Bi. Mwaipopo anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Dkt. Luhende ambaye ametuliwa kuwa Wakili Mkuu wa Serikali.​
Uteuzi huu umeanza tarehe 09 Oktoba, 2022.

Uteuzi.jpg
 
Hiki cheo cha wakili mkuu wa serikali alikianzisha Magufuli, baada ya kuona serikali inashindwa kesi kila mara chini ya mawakili wake.

Natamani kujua miaka zaidi ya miwili baada ya uwepo wa hicho cheo, serikali imepata mafanikio gani kuhusu kesi zilizokwenda mahakamani, wameshinda ngapi?

Na iwe wameshinda kihalali, pasiwepo na undue influence toka upande wowote hasa kwa hao mahakimu wanaotaka kuteuliwa kuwa majaji, hivyo wanaogopa kumkasirisha bosi wao.
 
Kwamba alikuwa "Wakili Mkuu wa Serikali", sasa anakwenda kuwa "Naibu Wakili Mkuu..."!
Nadhani kwa kiingereza ingeeleweka vizuri zaidi:
Wakili Mkuu wa serikali= Attorney General;
Naibu Wakili Mkuu wa serikali= Deputy Attorney General; na
Wakili wa serikali Mkuu= Principal Attorney
 
Nadhani kwa kiingereza ingeeleweka vizuri zaidi:
Wakili Mkuu wa serikali= Attorney General;
Naibu Wakili Mkuu wa serikali= Deputy Attorney General; na
Wakili wa serikali Mkuu= Principal Attorney

Hii sio tafsiri sahihi.[emoji1426]

Tafsiri sahihi ni hii [emoji1541]

Wakili Mkuu wa Serikali = Solicitor General

Naibu Wakili Mkuu wa Serikali = Deputy Solicitor General

Mwanasheria Mkuu wa Serikali = Attorney General

Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali = Deputy Attorney General
 
Nadhani kwa kiingereza ingeeleweka vizuri zaidi:
Wakili Mkuu wa serikali= Attorney General;
Naibu Wakili Mkuu wa serikali= Deputy Attorney General; na
Wakili wa serikali Mkuu= Principal Attorney
No, umechanganya mambo kidogo...!

Kwani Attorney General (AG) ndiye "Wakili Mkuu wa Serikali" kwa lugha ya Kiswahili..?

Kama ndivyo, Je, kuna tofauti yoyote kati ya "Mwanasheria Mkuu wa Serikali" ambaye ndiye tunamjua kwa kiingereza kama "Attorney General - AG" na "Wakili Mkuu Mkuu wa Serikali" kwa kiingereza akijulikana kama "Solicitor General..?"
 
Vyeo vingine bhana !
Yaani vinachekesha kweli. Ebu fikiria, mtu anakuwa Makamu Mwenyekiti wa Chama na kipindi chote cha uongozi wake yupo nje ya nchi. Kazi anafanya saa ngapi sasa. Yaani vyeo vingine havina maana kabisa!!
 
Back
Top Bottom