Rais Samia afanya uteuzi wa viongozi mbalimbalia, pia amevunja Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF)

Katika hatua nyingine, Rais Dkt. Samia ameivunja Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Taifa wa

TOKA MAKTABA :
16 March 2025

MWENYEKITI WA BODI YA WADHAMINI YA NSSF AMSHUKURU RAIS DKT. SAMIA KWA KUWAAMINI KUONGOZA BODI HIYO​

​

Na MWANDISHI WETU,​

Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Bi. Mwamini Malemi, amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuwaamini kuongoza Bodi hiyo, ambapo ameahidi kuendelea kufanya kazi kwa kufuata sheria, sera na taratibu.​

​

Bi. Mwamini amesema hayo mwishoni mwa wiki wakati wa uzinduzi wa Bodi ya Wadhamini ya NSSF, jijini Dar es Salaam, ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Mhe. Ridhiwani Kikwete, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu.​

​

Amesema dhamana waliyopewa Bodi ya Wadhamini ya NSSF ni kubwa hivyo watahakikisha wanatekeleza majukumu yao kwa kushirikiana na Menejimenti, Ofisi ya Waziri Mkuu, wadau mbalimbali wakiwemo wa UTATU ili kuhakikisha Mfuko unazidi kuwa imara.​

​

"Tumepokea maelekezo yako na tunaahidi kuyafanyia kazi na kuyatekeleza yote ili yaweze kuleta tija katika Mfuko," amesema Bi. Mwamini.​

​

Naye, Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Bi. Mary Maganga amewataka Wajumbe wa Bodi kusimamia Mfuko kwa uadilifu na kuzingatia maslahi mapana ya wanachama.​

​

Akizungumza wakati akizindua Bodi hiyo, Mhe. Ridhiwani amewapongeza Wajumbe wa Bodi na amewataka wafanye kazi kwa kufuata sheria, taratibu, kanuni na miongozo inayotolewa na Serikali.​


View: https://m.youtube.com/watch?v=lEe2LYcQmxQ​

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Bw. Masha Mshomba aliwaahidi Wajumbe wa Bodi hiyo kuwapa ushirikiano mkubwa ili waweze kutimiza majukumu yao kwa mujibu wa sheria.​



Bodi hiyo inaongozwa na Mwenyekiti wake, Mwamini Malemi wajumbe wake Oscar Mgaya, Lucy Chigudulu, Abdul B. Zuberi, Masha J. Mshomba, Juliana Mpanduji, Joseph S. Nganga, Fauzia Malik na John Kinuno

Board Of Trustees​

Board Chairperson​


Mwamini J. Malemi​

Board Chairperson

Board Secretary​


Masha J. Mshomba​

Board Secretary

Board Member​


Abdul B Zuberi​

Vice Chairman of the Board

Juliana C. Mpanduji​

Board Member

Joseph S. Nganga​

Board Member

John Kinuno​

Board Member

Hery H. Mkunda​

Board Member

Fauzia A. Malik​

Board Member

Lucy W. Chigudulu​

Board Member

Oscar P Mgaya​

Board Member
 
Mtamsingizia bure mama wa watu yeye analetewa tu list anaambiwa wateue hawa basi
 
Kwa hiyo amevunja board ili milango ya uchotaji iwe rahisi na tutegemee uteuzi baada ya uchaguzi.
Hakuna kitu kama hicho. Unadhani hela kuchotwa NI Rahis kihivyo. Amevunja Ili muendelee kuwa Na ufanis.
 
Bodi ya nssf imedumu miez 4 TU madarakani 😭

Hatari sana kwa maendeleo endelevu ya mashirika ya umma.

Pengine bodi ya NSSF ilikataa kuchangia fedha kusaidia chama dola kongwe, au uteuzi wa wajumbe ulifanyika bila vigezo vya uwezo n.k Taarifa hii inazua maswali mengi yasiyo na majibu.

ila Reforms zinatakiwa, ili wanachama wanaokatwa mapato yao kuchangia mfuko wa NSSF ambao ndiyo Wadau Wakubwa waelezwe sababu kinaga ubaga za bodi kuvunjwa na pia uteuzi unapofanyika wanachama wa mfuko NSSF waelezwe uwezo wa wajumbe wa bodi
 
Huyu bibi tuandamane tu na kumtimua pale ikulu
 
Kuna watu foreign watakuwa wanaloga hiyo gig ya kubwa wapewe wao. Ina maana raisi bado atambui kujiuzulu kwa Polepole bila ya barua rasmi kwenda serikalini ama?

Kuna sababu gani nyingine za kuacha wazi nafasi ya Cuba ukizingatia staili yao Ikulu ni kuapisha wanaoteuliwa kwa mkupuo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…