Rais Samia afanya Uteuzi wa Wakuu wa Mikoa na Taasisi: Hamduni-TAKUKURU, Makala-Dar, Kafulila-Arusha, Chalamila-Mwanza, Sendiga-Iringa, Makongoro...

Rais Samia afanya Uteuzi wa Wakuu wa Mikoa na Taasisi: Hamduni-TAKUKURU, Makala-Dar, Kafulila-Arusha, Chalamila-Mwanza, Sendiga-Iringa, Makongoro...

Mama ilimradi tu afanye lolote aongolewe kwa miaka watu walikuwa wanalalama kubadilisha badilisha wakuu wa mikoa na wilaya kunaondoa consistencies ndio maana Magufuli aliwaacha.

Hao watu kwa muda waliokaa wanafahamu changamoto za maeneo yao, plan zilizokuwepo na changamoto za watendaji wao.

Kingine Magufuli for once alijitahidi kuweka wakuu wa mikoa kutokana na maeneo wanayoyafahamu au skills zao ili watatue changamoto kutokana priority wanazozifahamu wao.
pole sana mkuu......naona unapinga. hongereni!!
 
Plan za Kisarawe zinawekwa na Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe na zinasimamiwa na DED sio Jokate anayeuza sura kwenye Marathon na kina Shilole.
Nipate tabu ya nini, kubadilisha badilisha watu kunaondoa consistency.

Chukulia mtu kama Jokate ana plan zake kibao Kisarawe kesho umtoe umpleke sijui Rukwa si anaenda kuanza upya tena, huyo atakaenda huko ataendeleza legacy zake?

Kubadilisha badilisha watu vituo vya kazi ni mambo ya kishamba tu.
 
Pia kumbuka Byakanwa ndiye aliharibu shamba la Mbowe kuharibu miundombinu kapata malipo yake kama sabaya sasa anatakiwa alipe
 
Mtaka ni RC makao makuu Dodoma. Mzee Mahenge amepelekwa Singida, Mzee Makongoro Nyerere yumo wakati huo huo tumeambiwa Eng. Ndikilo ni mzee, umri umepitia na amestaafu. Umri wa Makongoro na Mahenge ni mdogo kuliko Ndikilo?

Hizi teuzi baada ya kutaja jina wangeweka umri. Hapo tungepata picha wana umri gani na watastaafu lini
 
Plan za Kisarawe zinawekwa na Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe na zinasimamiwa na DED sio Jokate anayeuza sura kwenye Marathon na kina Shilole.
Mbona wengine hawakufanya kama rahisi ivyo. Kisarawe ilikuwa ina attention leo kama ilivyo sasa chini ya Jokate au we mwenye si ajabu huo msitu wa kazimzumbwi umeujua kupitia ushoroba festival.
 
Asante sana mama Kwa kukukumbuka familia ya Mwasisi wa Taifa letu, Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere kwa vitendo kwa kumteua Makongoro.

Mungu akubariki mama Samia.
 
Hizo ni kazi za kawaida sana, hakuna cha ajabu.
Mkuu wa JKT Gen Kabuge vipi tena anaondolewa.? Jamaa amesimamia Ujenzi wa ukuta, ujenzi wa Ikulu, na miradi kibao hadi akapandishwa cheo mbele na magufuli.
 
Back
Top Bottom