Rais Samia afanya Uteuzi wa Wakuu wa Mikoa na Taasisi: Hamduni-TAKUKURU, Makala-Dar, Kafulila-Arusha, Chalamila-Mwanza, Sendiga-Iringa, Makongoro...

Rais Samia afanya Uteuzi wa Wakuu wa Mikoa na Taasisi: Hamduni-TAKUKURU, Makala-Dar, Kafulila-Arusha, Chalamila-Mwanza, Sendiga-Iringa, Makongoro...

Wakuu mimi si mjuzi wa kila kitu hivyo vingine nitoe kwenu Wajuzi.
Je, anacho fanya Rais Samia suluhu ni uteuzi au uhamisho wa kazi.
Kwa jinsi nilivyo ona ni kua taarifa zinatoka hivi.
"Rais Samia amemteua Fulani kua mkuu wa mkoa fulani, akichukua nafasi ya fulani aliye hamishiwa mkoa fulani. Awali fulani alikuwa mkuu wa mkoa fulani"
Je, huo ni uteuzi au uhamisho. Maana ukiangalia uteuzi kafanya kwa wachache kama Sendinga ila wengine naona kama uhamisho tu.
Tujuzane kwa hilo.

AMETEUA WACHACHE SANA ILA WENGINE KAHAMISHA..AMESHINDWA HATA MUPA URC YULE WAZIRI KAIRUKI
 
Ingekuwa mkeka wa JPM, Wachagga wangelalamika kwamba wanabaguliwa. Ila kwa sababu ni mkeka wa mama SSH inabidi waugulie ndani kwa ndani.
Watasubiri sana, wanachuki sana wale system ilishawajua
 
Umeshawahi kufika Tabora?
Iringa ndiyo inalisha Tabora?
Hizi dharau kwa mikoa mingine mnazitoaga wapi?
Nenda Tamisemi site yao Tabora ni moja wapo ya mikoa maskini sana Tanzania sio maneno yangu hizo ni takwimu za serikali. Iringa, Ruvuma, Rukwa mikoa ya kusini inajulikana katika uzalishaji wa chakula nchi hii.
 
Unaondoa consistency utendaji kazi unakuwa imara zaidi watu wanapoanza kuelewa strength na weakness za wenzao, tabia za wenzao ili wasikwaruzane na waende vipi pamoja kupanga mipango yao ya muda mrefu.

Nina uhakika Mtaka alikuwa bado na plan zake kibao Simiyu au Chalamila na vita vyake na wafugaji kuingia mbugani Mbeya.

Unawabadilisha wanaenda kuanza na vipaumbele vipya, hiyo inaondoa consistency kwenye kazi na priority za maeneo.

Chukulia mtu kama Jokate na plan zake za kuifanya Kisarawe ichangamke mtu atakaefuata si anaenda achana na plan yote.
Mkuu wa mkoa anapangiwa vipaumbele kumbe?
 
Naona Kafulila na Makongoro wamekumbukwa!

Ally Hapi nae bado anakumbukwa!

Kulikoni Bosi wa TAKUKURU kupangiwa kazi nyingine!
Makongoro Nyerere sasa abadilike, akue na ajue hiyo ni Keki yake ya mwisho Mama amempa aile baada ya Kuwaangusha akina Hayati Mkapa, Mzee Kikwete na hata Hayati Magufuli ambao walimbeba kwa kila namna ila akawa habebeki kwa tabia zake za Utoto ( Ujana ) japo sasa ni Mtu mzima.

Nimefurahi kusikia ameteuliwa na kuwa Manyara RC sasa na namtakia Kila Ia Kheri katika hayo Majukumu yake mapya na makubwa ya Kimkoa.
 
Du. Jiwe alikuwa na nia njema sana na nchi yenu. Shida kubwa. Nyie wote wapiga domo hamjui hata nchi kama Tz. Inataka Nini kwa wakati gani. Ukiona unamwelewa sana kiongozi ujue Kuna Shida. Rais sio katibu kata anayefanya kila kitu mwenyewe. Mnapoandika Ni kama vile Rais anafanya yote kwa knowledge binafsi.
Umejieleza vizuri kuwa sio mtanzania!
Mambo ya Tanzania tuachie wenyewe!

#PILIPILI ISIYOYAKO INAKUWASHIA NINI??
 
Wakuu mimi si mjuzi wa kila kitu hivyo vingine nitoe kwenu Wajuzi.
Je, anacho fanya Rais Samia suluhu ni uteuzi au uhamisho wa kazi.
Kwa jinsi nilivyo ona ni kua taarifa zinatoka hivi.
"Rais Samia amemteua Fulani kua mkuu wa mkoa fulani, akichukua nafasi ya fulani aliye hamishiwa mkoa fulani. Awali fulani alikuwa mkuu wa mkoa fulani"
Je, huo ni uteuzi au uhamisho. Maana ukiangalia uteuzi kafanya kwa wachache kama Sendinga ila wengine naona kama uhamisho tu.
Tujuzane kwa hilo.
Uko sahihi kabisa kwa sehemu kubwa mama kafanya uhamisho
 
Back
Top Bottom