Rais Samia afanya Uteuzi wa Wakuu wa Mikoa na Taasisi: Hamduni-TAKUKURU, Makala-Dar, Kafulila-Arusha, Chalamila-Mwanza, Sendiga-Iringa, Makongoro...

Mbona kuna wazee wengi wa kiteuliwa kama Mkuchika why Makongoro asiteuliwe?

..at least mkuchika ana rekodi ya kutumikia kwenye ukuu wa wilaya, ukuu wa mkoa, na ni mbunge wa kuchaguliwa.

..sasa hebu niambie makongoro ana kitu gani special mpaka ateuliwe ktk umri wa kustaafu.

..na wakati huohuo kuna wakuu wa mikoa kama mghwira, na zambi, imeripotiwa kwamba wameachwa kwasababu wamefikisha umri wa kustaafu.
 
Chalamila anaendelea kupeta tu Dah!

Chalamila na Happi hawana budi kujitathmini utendaji wao kwani naona wameachwa kiporo ili mama asionekane kuwa hayuko na Mwendazake!!! Wakiendelea na using wao waliokuwa wanafanya enzi za Mwendazake siku si nyingi watakwenda na Maji!
 
Sasa Hamduni hapa pake. Amekuwa kwenye Kitengo cha Intelijensia na upelelezi pale Makao Makuu ya Polisi kwa miaka ya kutosha. Na alifanikisha misheni nyingi kwa muda aliokaa pale. Kwangu mimi kwa jinsi ninavyomfahamu anastahili hiyo nafasi
Intelijensia na Upelelez toka lini??? Hao ni watu wawili tofauti ambao hawaivagi chungu kimoja na hata siku moja hawaingiliani
Hamduni ni CID-Interpol-akarudi kwa manumba

Polisi intelijensia hajawahi kuwa
 
Acha ukabila Ndugu jenga hoja.
Nitajie Wabunge wa Jiji la Dar ambao ni Wazaramo,Wangindo,Wandengereko ambao ni Wabunge.
Watanzania popote walipo wanarusiwa kugombea uongozi wowote usipende kushambulia makabila ya Watu kwani kujiaribia tu Ndugu
 
Hongera Hamduni.....najua wewe sio mtu wa visasi...Kangi Lugora utamuacha tu na ulishamsamehe
 
..mama angeleta watu wapya siyo wazee wahenga kama makongoro nyerere.
Kwenye hivyo vyeo kuna mambo mengi ya kimkakati.
Kuna wanaoteuliwa kuleta Suluhu za kiuchumi, kukomesha vurugu mahali husika, kuimarisha usalama nk.
Kuna watu wanateuliwa mahali kuvunja nguvu za mitandao ya kisiasa ya ndani kwa ndani CCM ili ikibidii kupandikiza na kuimarisha mitandao inayohitajika.

Kwahiyo usishangae kuona wazee kama Makongoro kwenye baadhi ya maeneo.
 
Mkuu mbona sasa kama unachonganisha. Utumishi wa Umaa siku hizi ndivyo ilivyo, leo wewe, kesho utapangiwa kazi na junior officer wako wa jana. So you are suppose to be smart always.
 
Hakuna kitu pale ni zawadi tu kama ya happy birthday
 

..kama ni kweli, basi hayo yatakuwa ni matumizi mabaya ya madaraka, na fedha za umma.
 
Nimepitia orodha ya wakuu wa mikoa waliochaguliwa na Mh. Samia Suluhu. Kwa mkoa wa Manyara ulivyo nyuma kimaendeleo kupewa Makongoro Nyerere kuwa mkuu wa mkoa huo ni rasmi kuwa upinzani umefunguliwa mlango wa kuambiwa karibu Manyara.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…