Rais Samia afungua Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Chama cha Mahakimu na Majaji Tanzania (TMJA)

Rais Samia afungua Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Chama cha Mahakimu na Majaji Tanzania (TMJA)

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,352
Reaction score
15,876
Rais Samia akifungua Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Chama cha Mahakimu na Majaji Tanzania (TMJA) katika viwanja vya Makao Makuu ya Mahakama (Judiciary Square), mkoani Dodoma, leo Januari 13, 2026.


Jaji Mkuu George Mcheche Masaju amesema kuwa Mahakama sasa zinatumia Kiswahili, na kwamba hukumu pia zitaanza kutolewa kwa Kiswahili mara tafsiri za matoleo ya kisheria zitakapokamilika.

"Ufikiwaji wa Mahakama na lugha inayotumika ni jambo muhimu. Lugha tunayotumia ni Kiswahili; tumeshatoka kwenye matumizi ya lugha ya Kiingereza. Mhe. Rais, niseme Mwanasheria Mkuu wa Serikali, atakapokuwa amekamilisha tafsiri ya matoleo ya kisheria kwa lugha ya Kiswahili, tutaanza pia kutoa hukumu kwa Kiswahili."

"Nimeambiwa yupo hatua za mwishoni na sheria tayari ilishatungwa inayosema lugha ya Mahakama itakuwa ni ya Kiswahili"

"Mhe. Rais Mahakama haiwezi kuwa huru indapo Watendaji wake hawana uhakika wa Mishahara yao, Posho, Pensheni na Mazingira bora ya kazi"

Rais Samia Suluhu Hassan, amesema "Nitoe msisitizo kwamba kwa upande wetu Serikali, tutatimiza wajibu wetu wakuendelea kuimarisha huduma za Mahakama, lakini niwatake nanyi kutimiza wajibu wenu ndugu zangu Majaji na Mahakimu ambao ni kusimamia HAKI kwa kuzingatia KATIBA, SHERIA na MAADILI bila hofu, huba wala upendeleo na hiki ndicho kiapo chenu"

Soma zaidi
 

Attachments

Nani kama Samia? Tunajivunia sana kuwa na Rais Shupavu Miaka 10 tena kwa Rais Dr. Samia Suluhu Hassani​
 
Back
Top Bottom