Mgombea wa nafasi ya rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Samia Suluhu Hassana akizungumza na Wananchi katika Mkutano wa Kampeni za CCM uliofanyika leo, tarehe 18 Septemba, 2025, katika Jimbo la Nungwi, visiwani Zanzibar amesema ahadi za Chama cha Mapinduzi kwa Watanzania miaka mitano ijayo ni kutenda au kuendelea kukuza uchumi na kipato cha wananchi, kuinua hali za maisha ya Watanzania wote, kuimarisha ustawi wa jamii, kulinda amani, usalama na utulivu katika nchi yetu, vilevile kudumisha demokrasia na utawala bora na Muhimu zaidi kujenga Taifa linalojitegemea.
Ameeleza kuwa katika kujenga Taifa linalojitegemea kila kijana awe na shughuli inayompa kipato aweze kujitegemea na ndiyo kazi ambayo serikali inaendelea kufanya kuandaa mazingira kwa vijana na watanzania kuwa na shughuli ya kufanya ili waweze kuingiza kipato na kuinua uchumi wa Taifa.