Zack Abdul
JF-Expert Member
- Mar 9, 2026
- 1,194
- 911
Akizungumza katika Jukwaa la 29 la Kimataifa la Uchumi la St. Petersburg (SPIEF 2026) nchini Urusi leo Ijumaa, Juni 05, 2026, Dkt. Samia alisema kuanzishwa kwa safari hizo ni hatua muhimu katika kuimarisha uhusiano wa kiuchumi kati ya mataifa hayo mawili.
Aidha, ameeleza kuwa Tanzania inatarajia pia kuona shirika la ndege la Azur Air likianza safari za moja kwa moja kutoka Moscow kwenda Zanzibar.
Rais Samia amesema licha ya Tanzania na Urusi kuwa na historia ndefu ya ushirikiano na urafiki wa zaidi ya miongo sita, kiwango cha biashara kati ya nchi hizo bado hakilingani na ukubwa wa uhusiano wao.
Amebainisha kuwa biashara ya pande mbili mwaka 2025 ilikuwa chini ya dola nusu bilioni za Marekani huku Urusi ikichangia chini ya asilimia moja ya biashara yote ya Tanzania mwaka 2024.
Katika hotuba yake, Rais Samia amezitaja sekta tano zenye fursa kubwa za ushirikiano wa haraka kati ya Tanzania na Urusi kuwa ni madini, kilimo, nishati, mafuta na gesi pamoja na afya na dawa.
Amesema Tanzania ina rasilimali nyingi za madini ikiwemo dhahabu, urani, nikeli na madini muhimu ya kimkakati, huku ikiwahamasisha wawekezaji kushiriki katika utafiti wa kijiolojia na ujenzi wa viwanda vya kuchakata madini.
Pia amewaalika wawekezaji wa Urusi kuwekeza katika uzalishaji wa mbolea, uchimbaji wa mafuta na gesi, uzalishaji wa vifaa tiba na dawa pamoja na miradi ya nishati safi ikiwemo teknolojia ya vinu vidogo vya nyuklia.
Soma Pia: ATCL Kuanza Safari za Moja kwa Moja Tanzania-Moscow 2026
Akizungumzia mazingira ya uwekezaji nchini, Rais Samia amesema Tanzania ina zaidi ya watu milioni 61, uchumi unaokua kwa wastani wa asilimia sita kwa mwaka na mfumuko wa bei wa asilimia tatu, hali inayoiweka miongoni mwa nchi zenye ukuaji wa kasi zaidi barani Afrika.
Ameongeza kuwa Tanzania ni lango la soko la zaidi ya watu milioni 500 katika Afrika Mashariki na Kusini.
Rais Samia amehitimisha kwa kuwataka wafanyabiashara na wawekezaji kutoka Tanzania na Urusi kuhamia kutoka kwenye mazungumzo kwenda kwenye utekelezaji wa miradi halisi yenye manufaa kwa wananchi wa mataifa yote mawili, huku akisisitiza kuwa Serikali ya Tanzania itaendelea kuweka mazingira bora ya biashara na uwekezaji.
Pia soma ~ ATCL: Tumesitisha safari ya Dar - Moscow kutokana na vihatarishi vya mazingira ya uendeshaji