Rais Samia aizawadia Taifa Stars Tsh. Milioni 200 kuelekea mechi na Morocco

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amewazadia Taifa Stars shilingi milioni 200 kuelekea mchezo wa robo fainali dhidi ya Morocco, utakaochezwa Ijumaa, Agosti 22, 2025 katika uwanja wa Benjamin Mkapa, jijini Dar es Salaam.

Fedha hizo zimewasilishwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi, alipoitembelea timu hiyo kambini jijini Dar es Salaam, leo Agosti 20, 2025, na kuwapongeza kwa hatua kubwa waliyofikia pamoja na kuwatakia heri kwa mchezo ujao.

Swali fikirishi zawadi hutolewa wakati gani?

Gift VS Responsibilities

Nadhani hiyo ni motisha ama hamasa siyo zawadi kwa mtizamo wangu
 
hizi ni rushwa kama rushwa nyingine, kila kitu ni hela tu, hizi hela ni za kwenda kuhonga marefa na kuwapulizia wapinzani wetu dawa za kuwalewesha ili tusicheze kwa ushindani, HII CHAN inachezwa kwa maelekezo tu.
ni kama ile mechi ya RS Berkane ilivyokuwa ya maelekezo
 
halafu OKTOBA kuna watu wanafikiti ina tofauti wakatiwashajiweka BILIONI 86 za kuharibu uchaguzi!
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amewazadia Taifa Stars shilingi milioni 200 kuelekea mchezo wa robo fainali dhidi ya Morocco, utakaochezwa Ijumaa, Agosti 22, 2025 katika uwanja wa Benjamin Mkapa, jijini Dar es Salaam.

Fedha hizo zimewasilishwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi, alipoitembelea timu hiyo kambini jijini Dar es Salaam, leo Agosti 20, 2025, na kuwapongeza kwa hatua kubwa waliyofikia pamoja na kuwatakia heri kwa mchezo ujao.

Jambo Kubwa sana
 
Milioni 200 ni hela kubwa sana,mnaonaje hiyo hela nikamegewa hata milioni 2 tu nikaanza biashara nikajikwamua kutoka kwenye umasikini?
 
Pesa zinamwagwa tu, halafu wananchi wa nzovwe, mnivata, mkonjoano tandahimba wanajenga shule na vituo vya afya kwa nguvu zao. Hii nchi laana kabisa
 
Ruto anatoa zaidi ya hizo na wakenya walipambana haswa Sasa matokeo yameonekana
Hiyo hela ikiingia mfukoni kwa wachezaji Morocco kesho anakufa chuma 3 hata hivyo kesho ushindi lazima na itakuwa zawadi kwa mama
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amewazadia Taifa Stars shilingi milioni 200 kuelekea mchezo wa robo fainali dhidi ya Morocco, utakaochezwa Ijumaa, Agosti 22, 2025 katika uwanja wa Benjamin Mkapa, jijini Dar es Salaam.

Fedha hizo zimewasilishwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi, alipoitembelea timu hiyo kambini jijini Dar es Salaam, leo Agosti 20, 2025, na kuwapongeza kwa hatua kubwa waliyofikia pamoja na kuwatakia heri kwa mchezo ujao.

Sengerema Walimu intake mpya fedha za kujikimu hawajapewa tangu march , mbona prioritization kwetu ni mitihani. Sio vibaya kuwapa motisha lakni inaumiza kuona Kuna watu wanaovuja jasho kujenga mustakabali wa jamii Bora itakayojenga Taifa imara kupitia Wizara ya elimu wakisahauliwa Alafu kuna watu ndani ya week 3 wamevuna zaidi ya 200+ml 🥲
 
Back
Top Bottom