Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan Akitembelea Bandari ya Tanga na Kuzungumza na Wafanyakazi wa Bandari, leo tarehe 01 Machi, 2025.
---
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, leo Machi 1, 2025, ametembelea Bandari ya Tanga kukagua maboresho makubwa yaliyotekelezwa, yakiwemo ujenzi wa gati mbili mpya.
Akiwa bandarini hapo, Rais Samia amepongeza maendeleo yaliyopatikana na kusisitiza kuwa Tanga sasa inajidhihirisha kama lango muhimu la biashara kwa Afrika Mashariki na dunia kwa ujumla.
"Tulitamani kwa muda mrefu kuona meli kubwa zikitia nanga hapa, shughuli za bandari zikishamiri, na vijana wakipata ajira. Leo hii, ndoto hiyo imetimia kupitia uwekezaji wa Shilingi bilioni 429 katika maboresho haya," amesema Rais Samia.
Marekebisho hayo yameongeza kina cha maji bandarini, kuruhusu meli kubwa kufunga moja kwa moja kwenye gati badala ya kutumia matishari. Pia, muda wa kuhudumia meli umepunguzwa kutoka siku kadhaa hadi siku mbili pekee.
Tangu maboresho hayo kufanyika, uwezo wa Bandari ya Tanga kuhudumia mizigo umeongezeka kutoka tani 400,000 mwaka 2019/2020 hadi tani 1,200,000 hivi sasa. Hili ni ongezeko la zaidi ya tani 700,000. Aidha, mapato yameongezeka maradufu, kutoka Shilingi bilioni 17.27 hadi Shilingi bilioni 49 ndani ya miezi saba pekee ya mwaka huu wa fedha.
Rais Samia amesisitiza kuwa mafanikio haya hayatanufaisha tu wafanyabiashara, bali pia serikali kupitia ongezeko la mapato na kukuza sekta ya viwanda.
"Natamani kurudisha hadhi ya Tanga—iwe kitovu cha viwanda, bandari kubwa na eneo muhimu kwa uvuvi. Hiki ndicho ninachokifanya," amesisitiza.
Katika hatua nyingine, ametangaza mpango wa kujenga barabara ya Handeni-Kiberashi-Kijungu-Singida (KM 340) kwa mfumo wa ubia kati ya serikali na sekta binafsi (PPP), akieleza kuwa itarahisisha usafirishaji wa mizigo kutoka Bandari ya Tanga kwenda sehemu mbalimbali za nchi na kimataifa.
"Tutaiwekea road tolls ili mwekezaji anayejenga barabara hii aweze kurudisha gharama zake," amesema.
Akihitimisha hotuba yake, Rais Samia amewataka wafanyakazi wa bandari kuongeza ufanisi ili kuifanya Bandari ya Tanga kuwa miongoni mwa bandari bora duniani.
"Tunashindana na bandari za mataifa mengine. Tukifanya kazi kwa bidii na kupunguza gharama za uendeshaji, Tanga itakuwa kitovu cha biashara Afrika Mashariki," ameongeza.
Maboresho haya yanaimarisha nafasi ya Bandari ya Tanga kama kitovu cha biashara, yakichochea ukuaji wa uchumi wa Tanzania kwa kuifanya kuwa lango kuu la biashara kwa meli kubwa na kuunganisha nchi na masoko ya kimataifa.