Rais Samia akemea suala la siri za Serikali kuvuja mitandaoni

Siri zibaki jeshini huko kwenye mbinu za kivita sio kwenye kodi zetu.

Kukiwa na ubishi jinsi kodizetu zinavyotumika mambo ya wekwe wazi tujue nani wakumuwajibisha kwenye sanduku la kura.
 
Kuvujisha siri zinaua Taifa ni Ushujaa , Natoa wito kwa wazalendo wote wakiwemo mawaziri , manaibu , makatibu wakuu , tiss na wote mnaoshika hizo nyaraka zao za hovyo zifichueni na Mungu atawabariki sana , Amina
 
Hivi Siri za serikali Ni zipi?. Kuficha maovu au mabaya?. Kwanini mwananchi ambaye ni mwaajiri anafichwa Mambo?. Lazima kuwepo na uwazi wa Nini Ni Siri za serikali na zipi sio.
 

Serikali inaogopa sana mitandao kama mwiba
 
Mama mwenyewe anapenda habari za mitandaoni balaa., Juzi si amefumza yale majibizano ya simu ya Lukuvi na genge lake kutaka kugombea Uspika.,

Na yale majibizano ya kakaake Lukuvi na genge lake kwanza yalitua hapa JF naamini mama yupo hapa JF saa zote ana brows.,
 
Siri za serikali au siri zako binafsi? Kama unavyowatoa watu wako "hapo" kuwapeleka "kule" ili wakalinde maslahi yako "kule" ni siri za serikali au siri zako binafsi mkuu wetu?
 
Siri zipi zilizovuja, huku yote ni ya kawaida tu

Itakuwa ile barua ya jobo kujiuzulu ndo anaongelea!!! Alafu sijui kwann anataka iwe ni Siri wakati sisi wanchi ndo maboss zao.... lazima watupe mirejesho ya kila jambo au ndo anataka kupiga mnada kama bwana yule alivyosema? Na anataka iwe siri
 
Siri za serikali au siri zako binafsi? Kama unavyowatoa watu wako "hapo" kuwapeleka "kule" ili wakalinde maslahi yako "kule" ni siri za serikali au siri zako binafsi mkuu wetu
I'm flooded😊😊😊😊😊
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…